Wizara ya Afya kupitia katibu wake Mercy Mwangangi ametangaza jana Ijumaha kuwa idadi ya
waliothibitishwa kuambukizwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona {Covid-19} nchini Kenya
imeongezeka na kufikia
2,474.Akitoa taarifa ya siku kutoka kwa wizara kuhusu maambukizi mapya, Dkt. Mwangangi amesema watu 3,177 wamepimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita huku 134 wakithibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
Waziri huyo ameongeza kwa kusema kwamba watu 90, 875 wamefanyiwa vipimo nchini humo hadi kufikia Juni 5.

0 Comments