Klabu ya Simba SC imeweka hadharani viingilio vya mchezo wao wa kirafiki wa kilele cha Simba Day dhidi ya TP Mazembe utakaofanyika Septemba 19, 2021 utapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kupitia kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Simba wamesema kuwa tayari vituo 11 vimeanza kuuza tiketi za tamasha hilo ikiwepo makao Mkuu ya klabu hiyo.
Mzunguko - 5000/=
VIP B & C - 20, 000/=
VIP A - 30, 000/=
Platinum 200, 000/=
Kikosi cha wachezaji 23 wa TP Mazembe kinatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumamosi kwaajili ya kuwakabili na mabingwa wa Tanzania.
0 Comments