TANGAZA NASI

header ads

MKURABITA wapongezwa kwa urasimishaji,wakutana na kilio cha umeme Njombe

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wamiliki wa viwanda mkoani Njombe wamelilalamikia shirika  la umeme Tanzania (TANESCO) kuwa linawasababishia hasara kubwa katika uzalishaji kutokana na umeme kukatika mara kwa mara huku wakirudisha nyuma jitihada za urasimishaji wa biashara za wanyonge.


Kwa mujibu wa wanufaika wa Mkurabita  ni kwamba biashara kubwa ambazo zimeathirika zaidi ni viwanda vya mikate,unga na bidhaa nyingine za chakula na biashara ambapo wameomba hatua madhubuti za kudhibiti ukatikaji zinatakiwa kuchukuliwa haraka iwezekanavyo ili kunusuru mitaji yao.


Vaileth Longo,Lucy Kitavile na Yona Chaula ni baadhi ya wajasiriamali ambao wametoa kilio chao mbele ya mkutano wa wajumbe wa mpango wa kurasimisha biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA uliofanyika mjini Njombe kwa lengo la kupata tathmni ya wanufaika ambapo wanasema wamejikuta katika wakati mgumu na kupata hasara kubwa kwa ukatikaji wa umeme uliokithiri.


“Tunashindwa kusogea mbele kwasababu ya umeme mimi na mwaga mikate kila siku na kuna kaka huwa anakuja kubeba kila siku yeye anafuga kuku”alisema Vaileth Longo


“Natamani nilie kutoka tarehe 27 mwezi wa kwanza sijafanya kazi kwasababu ya umeme,ninapata shida kubwa kwasababu ya umeme”alisema Lucy Kitavile


Akitolea ufafanuzi kuhusu changamoto zilizopo na hatua zinazochukuliwa mjumbe wa bodi wa mkurabita ambaye ni mkurugenzi wa sera na mipango wizara ya nishati Haji Janabi amesema Njombe haina upungufu wa umeme lakini ili kujua tatizo kwa kina anakwenda kukutana na meneja wa tanesco mkoa huku akifafanua kuwa mipango serikali kwa mkoa wa Njombe juu ya nishati ni mikubwa kwa kuwa ni mkoa wa kimkakati na serikali imeanza ujenzi wa miradi ya umeme kupitia maporomoko ya maji yam to Rumakali uliopo wilyani Makete na mto Ruhudji uliopo mjini Njombe.


“Niombe radhi sana kwa wale wadau wetu ambao wanachangamoto za nishati,kwa ujumla TANESCO inapaswa kuhakikisha kuna nishati ya kutosha ili wale wenye shughuli zao za kuendeleza maendeleo yao yaweze kwenda vizuri.Mkoa huu unategemewa kuzalisha megawati 1000 na tutaanza na megawati 580”alisema Haji Janabi 


Wakati jitihada za kutafuta suruhisho la kukatika kwa umeme mjini Njombe mtendaji mkuu wa Mkurabita Dr Selapia Mgembe na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi katika taasisi hiyo Daniel Ole Njoolay nao wanawahimiza wananchi kufanya urasimishaji wa mashamba na viwanja ili kuwapata hati ambazo ni ulinzi na hitaji muhimu kwenye mikopo ya taasisi za kifedha.


“Urasimaishaji ni mchakato lakini ni lazima uanze kichwani mwako kwa kusema nataka nianze kufanya mabadiriko ya kwangu binafsi kwa kuwa halmashauri zetu zina fursa za maendelep”alisema  Dr Selapia Mgembe


 


Post a Comment

0 Comments