TANGAZA NASI

header ads

Lango la Mpaka wa Rafah lafunguliwa



 Lango la Mpaka wa Rafah, lililoko kati ya Misri na Ukanda wa Gaza, ulio chini ya kizuizi cha Israel, lilifunguliwa njia zote mbili kwa siku nne.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Kitaifa huko Gaza, ilielezwa kuwa mabasi ya abiria yalianza kuondoka Gaza kupitia Lango la Mpaka wa Rafah, ambalo lilifunguliwa njia zote mbili.

Taarifa hiyo ya wizara pia ilibainisha kuwa uvukaji kupitia lango la mpaka uliofunguliwa kwa hali ya kipekee utaendelea kuanzia leo hadi siku ya Alhamisi Februari 4.

Lango la Mpaka wa Rafah, ambalo lilifungwa njia mbili kama tahadhari ya kupambana na janga la corona (Covid-19) mnamo mwezi Machi, mara kwa mara hufunguliwa kwa siku chache na kufanya kazi kwa sehemu ndogo.

Post a Comment

0 Comments