TANGAZA NASI

header ads

Maji ya bahari yabadilika rangi na kuwa nyekundu

 


Katika hali isiyo ya kawaida maji ya bahari iitwayo Dead sea iliyopo karibu na jangwa la Judea nchini Israeli yamebadilika rangi hii leo na kuwa rangi nyekundu kabisa kama damu.


Bahari hiyo yenye maajabu mengi yakiwemo kusaidia watu kuelea, yaani ukiwa ndani ya bahari hiyo unaelea tu huzami.


Bahari hiyo yenye kiwango kikubwa cha chumvi kufikia mara 9 ya kiwango cha chumvi cha bahari zingine kubwa imebeba historia nyingine haswa kwa waumini wa dini ya Kikristo kwani maandiko ya Biblia yanasema kuwa, Mungu alituma malaika zake kwenda ndani ya eneo linalopakana na bahari hiyo na kuharibu Sodoma na Gomorrah.


Mpaka sasa, vyombo vya usalama havijathibitisha bado ni kwanini maji ya bahari hiyo ndogo yamegeuka rangi lakini watu wanaamini kuwa ni kwa sababu ya maji hayo kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya chuma, wengine wanaamini ni kwa sababu ya bainowuai kama viumbe ambao wanaweza kuwa wamesababisha kubadilika kwa rangi.


Pamoja na hayo yote, bado kuna baadhi ya watu wanaotupa lawama kwa serikali ya Jordan kwa kushindwa kuzuia utupaji wa taka ovyo ndani ya bahari hiyo.


Tayari wizara ya maji na umwagiliaji ya Jordan imechukua sampuli za maji hayo kwa ajili ya uchunguzi zaidi lakini mkurugenzi wa kilimo kusini mwa bonde la Jordan Yassin al-Kasasbeh ameliambia shirika la habari la Roya kuwa maji hayo yamebadilika rangi kutokana na aina ya baktaria na viumbe wekundu wanaopenda hali ya chumvi chumvi katika uwepo wa mwanga wa jua.


Lakini nadharia yake bado haitoshi kuelezea ni kwanini sehemu tu ya bahari hiyo yaani baadhi ya vidimbwi ndiyo vilivyobadilika rangi wakati vingine vikibaki na rangi ya kawaida.


Dead sea imekuwa ikikumbwa na ukame ulisababisha maji kukauka sana ndani ya miaka ya hivi karibuni na sasa lina urefu wa maili 31 na upana wa maili 9 huku kina cha maji cha bahari hiyo kikipungua kutoka futi 131 na sasa kinapungua kwa futi mbili kila mwaka.

Post a Comment

0 Comments