Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi), anayeshughulikia elimu, Mwita Waitara ameagiza viongozi wa Mikoa ,Wilaya na uongozi wa shule za kidato cha sita kuchukua tahadhari zote za afya ikiwemo wanafunzi wa bweni kulala kwa umbali ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya corona.
Tahadhari zingine ni kuhakikisha wanafunzi na walimu wanavaa barakoa na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka kwenye maeneo yote ya kuingilia shuleni.
''Kuna uwezekano wazazi wakaingia gharama kidogo maana wanapaswa kuwanunulia barakoa, lakini na watakaoweza kuwanunulia vitakasa mikono ili kujikinga na ugonjwa wa corona.
Amesema waalimu waandae wanafunzi kisaikolojia ili wafanye vizuri kwenye mitihani yao.
Wanafunzi wanaweza nkwenda na tangawizi na hata kujifukiza pia ruksa na wanafunzi wote lazima wapimwe joto". alisema.
0 Comments