Dodoma.
Zaidi ya
tani 100,000 za mazao mbalimbali kutoka kwa wakulima wa ndani zimenunuliwa na
kuuzwa kwenye nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini kupitia
bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.
Akitoa
taarifa hiyo jijini Dodoma mkurugenzi mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko
DK Anselim Mushi amesema biashara hiyo imefanyika kwa kipindi cha
miezi minne iliyopita na kutengeneza Serikali faida ya zaidi ya Sh3.2 bilioni.
DK Mushi
amesema bodi hiyo inatarajia kununua tani za ziada 300,000 kwa ajili ya
kuziuzia katika nchi za Afrika Mashariki.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema hatua hiyo imeongeza soko la
uhakika kwa wakulima huku akiitaka bodi ihakikishe kunakuwepo na usalama wa
chakula nchini.
Mbali na
Naibu Waziri Mgumba kuitembelea bodi hiyo pia ametembelea kituo cha utafiti wa
kilimo cha Hombolo jijini Dodoma na kujionea uzalishaji wa mtama, uwele na
zabibu mazao ambayo yanayostahimili ukame.
0 Comments