WAKULIMA wa zao la Mpunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga
wamesema kuwa huenda mazao yao yakaozea shambani kutokana na ukosefu wa
barabara hali ambayo inapelekea vyombo vya usafiri kushindwa kufika katika
maeneo hayo katika kipindi hiki cha mavuno.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Nyanhembe Agricultural Farm
inayojishughulisha na shughuli za Kilimo na Ufugaji Khamis Mgeja amesema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea shamba lake la
mpunga lililopo katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago halmashauri ya Mji
wa Kahama Wilayani .
Pia Mgeja ameipongeza serikali kupitia wizara ya kilimo chini ya
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wa kumkomboa mkulima
kwa kutoa maelekezo ya kulielekeza shirika la Taifa la kuhifadhi chakula (NFRA)
kuanza kununua mazao mbalimbali msimu huu na kuacha mazoea ya kununua zao moja
tu la mahindi.
Baadhi ya wakulima katika Kijiji cha Nyanhembe Wilaya ya Kahama
akiwemo Salima Kazinza na Emmanuel Masebu Wamesema hali ya mwaka
huu imekuwa tofauti na mwaka uliopita hasa katika suala la uvunaji ambapo
karibu mashamba yote ya mpunga yana maji pamoja na njia za kwenda shambani
hivyo wao wamekubaliana na hali na hawana jinsi huku wakibainisha kuwa mwaka
huu umekuwa wa neema kwa kupata mazao mengi licha ya changamoto ya
kuyasafirisha kwenda nyumbani.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba
amesema halmashauri imekuwa ikiwatengenezea mazingira Rafiki wakulima ikiwa ni
pamoja na kuchimba mabwawa lakini changamoto iliyopo kwa sasa ni kuzidi kwa
kiwango cha mvua hata kwenye kipindi cha mavuno.
Wilaya ya Kahama ni miongoni mwa wilaya hapa nchini ambapo zao kuu la
chakula na biashara ni Zao la Mpunga likifuatiwa na zao la Mahindi ambapo pia
Wilaya hiyo iliyopo Mkoani Shinyanga ni maarufu kwa kilimo cha zao la tumbaku
nap amba pamoja na Uchimbaji wa Madini.
0 Comments