Na
Amiri Kilagalila,Njombe
Aliyewahi
kuwa katibu mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi,Mkuu wa Idara ya Sera na Itifaki
CHADEMA,Mjumbe wa kamati ya Ukawa na kampeni meneja wa Mgombea wa Makam wa Rais
Ukawa Bwana,Juju Martin Danda amepokelewa na Chama cha Mapinduzi CCM na
kukabidhiwa kadi ya Chama hicho na
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe.
Akizungumza
dhamira ya kujiunga na Chama hicho,Martin Danda amesema ni kutokana na uozo
uliopo katika vyama vya upinzani.
“Nilifanya
harakati nyingi sana katika kuvijenga vyama vya upinzani kwa maumivu makubwa na
umaskini mkubwa sana,tumeijenga Chadema tumeipeleka kwenye vyuo vikuu,lakini
kinachoendelea ndani ya vyama hivi ni
uozo wa hali ya juu ambao wengine tulishindwa kuvumilia”alisema Danda
Vile
vile amesema Vyama vya upinzani vimekuwa vinatengeneza wanaharakati wasiokuwa
na ajenda wanao shinda kutukana.
“Kuna
biashara ni vyama vinavyotengeneza wwanaharakati wasio kuwa na ajenda wanao
shinda kutukana,lakini ukizungumza chama cha kujifunza katika bara la
Afrika,namba moja ni Chama cha Mpainduzi”alisema tena Danda
Aidha
ametaka watanzania kuendelea kuunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Magufuli
kwa kuwa amefanya kazi kubwa kwa kuendesha miradi mikubwa huku akipongeza namna
hatua alizozichukuwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona na kuishangaza
Dunia.
Naye
katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole amesema kiongozi huyo sio
mwanasiasa wa kawaida kutokana na uvumilivu aliokuwa nao zaidi ya Chaguzi tano
akiwa Upinzani.
“Juju
Danda tumekwaluzana zaidi ya chaguzi tano yuko upinzani,na huku Njombe akiwa na
NCCR Mageuzi alikuwa na vijiji vichache na Vitongoji yote ilikuwa kazi ya huyu
bwana kwa hiyo ndani ya CCM naamini tumempata mtu mzuri,kwasababu ndiye
aliyepandikiza upinzani Njombe Kusini”alisema Erasto Ngole
Akizungumza
baada ya kumpokea na kumkabidhi kadi mwanachama huyo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Njombe Jassel Mwamwala,amesema wanakila sababu ya kuwapokea wanaorudi katika
Chama hicho kutokana na Nguvu waliyonayo iliyotengenezwaq na serikali ya awamu
ya Tano.
“Kwa
heshima ya viongozi wangu wa Taifa na kwa niaba ya wanachama wa mkoa wa
Njombe,nimempokea ndugu yetu Danda,na chama Cha Mapinduzi hakina Ubaguzi,hakina
Dini wala kabila wote tunaheshimiana kama ambavyo katiba inasema”alisema
Mwamwala
“Mwenzetu
hapa amesema vizuri kuwa amefanya kazi kubwa sana,amesema amefanya kazi kwenye
Ukawa,ameona kule hakuna amani,kuna uozo ndio maana amekuja kupata haki ya
uanachama kutoa mawazo yake”aliongeza Mwamwala.
0 Comments