Na Amiri kilagalila,Njombe
Chama cha Msalaba Mwekundu (RED CROSS TANZANIA)
wamezindua mpango wa utoaji elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya
Corona mkoa wa Njombe,ili kukata mnyororo wa maambukizi ya virusi hivyo nchini
Tanzania.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa zoezi hilo,Rais
wa Tanzania red cross Society David Kihenzile,amesema kwa kuwa serikali
ilishaanza kufanya kazi ya uelimishaji lakini wao kama Chama wameona haja ya
kuongeza nguvu kama wasaidizi wa serikali katika utoaji wa huduma za
kibinadamu.
Kihenzile amesema wanaendelea na zoezi hilo la
utoaji wa elimu karibu mikoa yote nchini huku mpaka sasa mikoa isiyozidi mitatu
ikiwa bado haijafikiwa na lengo likiwa ni kufikia mikoa yote nchini.
Amesema kwa mkoa wa Njombe wanakwenda kuvifikia
vijiji vyote 381 na mitaa yake 82 ili kuiongezea nguvu seriklai kwa ajili ya
kutoa elimu kwa jamii
“Tutakwenda kufikia katika mkoa wote wa Njombe kwa
maana wilaya zote na halmashauri zake sita,kata 107,tarafa 18,tutafikia vijiji
381 na mitaa yake 82,tutafikia maeneo ya umma na ya mikusanyiko ili kuiongezea
nguvu serikali kwenye kutoa elimu kwa jamii,na hatuendi kuongeza neon kwa kuwa
jumbe imeshapangwa na wizara ya afya kwa hiyo sisi tunaenda kupaza
sauti”alisema David Kihenzile
Simon M Kadogosa ni meneja Tathmini Magonjwa ya
Mlipuko kwa niaba ya Katibu wa Red Cross Tanzania,ameendelea kuwasihi
watanzania kupokea maelekezo ya wataalamu wa afya dhidhi ya kujikinga na virusi
vya Corona huku akibainisha kuwa miongoni mwa nyenzo watakazozitumia katika
kutoa elimu ni pamoja na mabango yenye jumbe za maandishi,vipeperushi pamoja na
vipaza sauti.
“Tutaunga mkono jitihada za serikali za utoaji elimu
kwa jamii kwa kuleta mabango 4000 yatakayobandikwa maeneo tofauti ndani ya
halmashauri zote kwa mpango jumuishi,tuna vipeperushi elfu kumi na nne pia
vitakavyogawiwa mkoa mzima,lakini pia watumishi wa kujitolea wa Red Cross
watatumia vipaza sauti kwenye maeneo ya kimkakati kuhakikisha zile jumbe za
sauti za watu wasio jua kusoma wanaziskia na kuzifanyia kazi”alisema Kadogosa
Naye Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri aliyekuwa
mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika ukumbi wa chuo kikuu huria
uliopo kwenye maeneo ya ofisi za mkoa wa Njombe,amesema mapambano ya Corona sio
viongozi bali ni kila mwananchi hivyo ni lazima kila mwananchi apambane huku
akifanya kazi.
“Elimu kwetu inaendelea lakini lazima tuamini
Mungu,na sisi huku tumeongeza nguvu kwa maneno matatu ya Sala,tahadhari na
kazi,na lazima tuchape kazi ili ugonjwa ukiondoka au ukiendelee tusije kujikuta
tupo kwenye anguko la kiuchumi”
Vile vile Ruth Msafiri ameendelea kuhamasisha watoa
huduma katika kusanyiko kuvaa barako huku akipiga marufuku kwa taasisi na watoa
huduma kuto kutoa huduma kwa mtu asiyevaa
barakoa wakati alipofuata huduma.
0 Comments