Taasisi isiyo ya kiserikali ya New Life Foundation ya mkoani Kilimanjaro imeanza kuhudumia kambi ya wazee iliyopo kata ya Mji mpya ikiwa ni sehemu ya Programu yake ya kuhudumia makundi mbalimbali yeye uhitaji hasa katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona.
Makundi ya Wazee,Watoto yatima na wale wanaoishi
kwenye mazingira magumu kwa sasa ni makundi yanayotajwa kutupiwa jicho la tatu
kutokana na hali ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona vinavyosababisha homa
ya Mapafu (COVID 19) .
Mkurugenzi wa New Life Foundation Baba
Askofu Glorious Shoo na Meneja Mradi wanasema taasisi yao
imeliona suala hilo na kuamua kuanzisha program maalumu kwa ajili ya
kungalia makundi ambayo yako kwenye hatari ya maambukizi ,ama walioko kwisha
pata maambukizi na wale wasio na uwezo wa kujikinga na maambuzki ya virusi vya
Corona .
Msaada wa vifaa hivyo pamoja na chakula vikakabidhiwa
kwa Afisa tawala wa wilaya ya Moshi ,Nathaniel Mshana ,kisha askofu wa kanisa
la Tanzania Assembless of God (TAG) ,Glorious Shoo
akasema msaada wa chakula pamoja na vitamins kwa ajili ya wazee hao
utakua ni endelevu.
Afisa tawala wa wilaya ya Moshi ,Nathaniel Mshana
akatoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada huo.
Kwa upande wake ,Mwenyekiti wa Mtaa wa Langoni
,Emeresiana Shirima pamoja na Mwakilishi wa wazee James Joseph
wanaolelewa katika kambi ya wazee ya Langoni wameshukuru taasisi ya New Life
Foundtion kwa msaada huo huku wakitoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano
huo.
0 Comments