TANGAZA NASI

header ads

Obama amkosoa Trump katika vita dhidi ya virusi vya Corona

 

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa namna anavyoshughulikia janga la Corona.Kauli yake ameitoa alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wake wa zamani kuungana na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden, televisheni ya CNN imeeleza

Ikulu ya Marekani imejibu kuwa hatua ya Rais “isiyo ya kawaida” ilikuwa “imeokoa maisha ya Wamarekani”.

Bw Obama alisema mbinu ya mrithi wake wa Republican kwa serikali ni sehemu ya kulaumiwa kwa namna alivyolishughulikia janga la Corona.

Bwana Obama pia amekosoa vikali uamuzi wa kufuta mashtaka dhidi ya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Michael Flynn.

Zaidi ya watu 77,000 wamepoteza maisha na Marekani sasa ina wagonjwa milioni 1.2 wa virusi vya corona, takwimu hizo zote ni za juu zaidi ulimwenguni.

Nchi nyingi ziliweka marufuku ya kutotoka nje mwezi Machi, lakini masharti hayo sasa yameondolewa, na kuruhusu watu kurudi kwenye shughuli zao.

Lakini maafisa wa afya wanaonya kuwa hatua hii inaweza kusababisha virusi kusambaa zaidi.itihada za Trump katika kupambana na virusi zimekuwa za nenda rudi.

Mwezi Februari alisema ugonjwa huu utatoweka, akitaka watu kuondokana na hofu lakini katikati ya mwezi Machi alieleza kuwa ugonjwa wa corona umekuwa ukisambaa kwa kasi nchini Marekani

Mwezi Aprili alipendekeza kuwa dawa za kuua bakteria zinaweza kuzuia virusi-jambo ambalo wanasayansi walilikana

Juma lililopita alitangaza kuwa atavunja kikosi kazi kinachofanya kazi ya kupambana na virusi vya corona, lakini baadae alisema wataendelea na kazi -lakini akielekeza kufungua uchumi wa nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments