Mamlaka za mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul zimeamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya virusi vya corona vinavyoibua wasiwasi wa kutokea wimbi la pili la kusambaa virusi hivyo hatari.
Meya
wa mji huo Park Won-soon amesema amri hiyo itakayoendelea bila kikomo
imefuatia maambukizi mapya ya virusi vya corona yaliyogundulika kwenye
wilaya ya Itaewon, yenye shughuli nyingi nyakati za usiku.
Zaidi
ya visa 24 vinahusishwa na mwanaume mmoja aliyegundulika kuwa
maambukizi ya COVID-19 baada ya kutembelea kumbi tano za starehe kwenye
wilaya ya Itaewon wiki iliyopita.
-DW
0 Comments