TANGAZA NASI

header ads

Mbunge aipongeza halmashauri ya Njombe kwa ukusanyaji mapato

 




Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mbunge wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe Edwin Swale ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa kufanikiwa kukusanya 56%  ya mapato ya ndani katika kipindi cha July hadi November wakati shughuli za madiwani zikiwa zimekasimiwa kwa watumishi katika kipindi hicho cha uchaguzi.


Swale ametoa pongezi hizo wakati akitoa salam katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani pamoja na uapisho kilichofanyika katika halmashauri hiyo.


Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa maendeleo wakati shughuli za maendeleo zikiwa zimekabidhiwa kwa watendaji wa halmashauri baada ya kuvujwa kwa baraza la madiwani.Mkurugenzi wa halmashauri Ally Juma amesema wamefanikiwa kuendeleza shughuli za maendeleo kikamilifu huku pia wakikusanya mapatao kwa asilimia 56%.


“Katika kipindi cha July hadi November 2020 halmashauri ya wilaya ya Njombe ilifanikiwa kukusanya bilioni 1,480,053,287/= sawa na asilimia 56% ya ukusanyaji katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani”  alisema Ally Juma


Aidha amesema halmashauri hiyo inakadilia kukusanya zaidi ya bilioni ishirini na nane,katika vyanzo vyake mbali mbali


“2020,2021 halmashauri ya wilaya ya Njombe imekadilia kukusanya Bilioni 28,279,875,66/=  kutoka kwenye vyanzo vyake mbali mbali vya mapato” alisema Ally Juma


Amesema katika vyanzo vyake vya ndani inatarajia kukusanya zaidi ya bilioni mbili


“Halmashauri inatarajia kukusanya bilioni 2,642,898,200/=  katika mapato yake ya vyanzo vya ndani”alisema tena Ally Juma


Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale ameipongeza halmashauri hiyo kwa hatua nzuri za ukusanyaji wa mapato na kusimamia kikamilifu matumizi ya mapato hayo.


“Kuna kiongozi mmoja wa serikali siwezi kumtaja ametoa sifa kubwa ya mkurugenzi kuongeza ubunifu wa ukusanyaji mapato ya halmashauri,kwenye hili nikupongeze sana na mimi pia,hii kwa kweli ni sifa kubwa na imekwenda mbali”alisema Mbunge


Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo akiwemo Oscar Kihombo amesema wanaamini sasa wanakwenda kufanya kazi za wananchi kikamilifu huku wakishirikiana katika zoezi la ukusanyaji wa mapato

Post a Comment

0 Comments