TANGAZA NASI

header ads

Wanafunzi 17,017 waliofaulu Njombe,wote kujiunga kidato cha kwanza

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe 


Wanafunzi 17,017 waliofaulu elimu ya msingi mkoani Njombe wote wanatarajia kujiunga na elimu ya sekondari kuanzia mwezi January kutokana na mkoa huo kujipanga na kuweka mazingira sawa ya miundombinu mashuleni na upokeaji wanafunzi.


Katibu tawala wa mkoa wa Njombe Catarina Revocat ameweka wazi idadi hiyo ya wanafunzi wanaopaswa kuanza elimu ya sekondari katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa Njombe kilichoambatana na uapisho wa madiwani pamoja na uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake huku akizitaka halmashauri zote kujipanga katika mchakato wa kuwapokea wanafunzi kwa kuwa hakuna mwanafunzi atakayeachwa.


“Tumefaulisha wanafunzi 17,017 elfu na wote wamepta nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza,hakuna hata mmoja aliyekosa nafasi ni lazima tuhakikishe wote wanaenda shule”alisema Catarina 


Amesema Rais Magufuli ameweka dhamira kwa kutoa elimu bure hivyo ni lazima wanafunzi hao wajiunge na elimu ya sekondari.huku akipongeza halmashauri zote za mkoa wa Njombe kwa ufaulu mzuri japo sio wa kuridhisha.


“Wanafunzi waliofanya mtihani 2020 Njombe tumefanya vizuri japo hairidhishi sana na tunahitaji kukaza buti zaidi kwa kuwa ni kawaida yetu Njombe kufanya vizuri”aliongeza Catarina


Halmashauri ya mji wa Njombe ni moja ya halmashauri inayofanya vizuri zaidi katika swala la elimu ndani ya mkoa wa Njombe hata katika takwimu za kitaifa.Kutokana na jitihada hizo taarifa ya mkurugenzi iliyotolewa kupitia makala ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ndani ya baraza la kwanza la madiwani imeonyesha utayari katika upokeaji wa wanafunzi kutoka na kukamilika kwa miundombinu mashuleni ukiwemo ujenzi wa madarasa pamoja na kuongezeka kwa shule mpya ya sekondari iliyopo kata ya Utalingolo itakayoanza kupokea wanafunzi kuanzia January 2021.


Erasto Ngole ni katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe akiwa katika baraza hilo ametoa rai kwa madiwani kwenda kushirikiana katika maendeleo ya halmashauri zao hususani ujenzi wa miundombinu kwa kuwa uchaguzi umekwisha.


“Madiwani nendeni mkawahamsishe wananchi wafanye kazi,tuache siasa za kulemba!  Ukianza kubembeleza wananchi hapa mwanzoni utafeli.Hapa mwanzoni watu wakujue kuwa diwani unapenda wafanye kazi”  alisema Erasto Ngole


Naye Ruth msafiri kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe ametoa rai kwa madiwani watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanasimamia zoezi la ufuatiliaji wa wanafunzi wote waliofaulu katika maeneo yao ili waweze kuingia darasani mapema shule zitakapofunguliwa


Post a Comment

0 Comments