TANGAZA NASI

header ads

Marekani kuwafikia wasichana zaidi ya 300 Makambako kuwapa elimu ya VVU



Na Amiri Kilagalila,Njombe


Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali inatarajia kuwafikia vijana wa kike kati ya miaka 14 hadi 25 zaidi ya 300 kwa mwaka 2021 kwa ajili ya kuwapa elimu ya VVU ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.


Zaidi ya wanawake 1033 kati ya 18759 ambao wamejitokeza kupima maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika halmashauri ya mji wa  Makambako wameripotiwa kukutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kipindi cha miezi kumi, kuanzia mwezi january hadi mwezi Octoba mwaka huu.


Kufuatia hali hiyo serikali kupitia mratibu wa uhamasishaji kwa wasichana kushiriki katika upimaji wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika halmashauri hiyo kwa ushirika wa shirika la Umbrela of  Woman and Disabled Organization (UWODO) imezindua mchakato wa kutoa elimu kwa vijana wa kike ikilenga kupunguza kasi  ya maambukizi mapya katika halmashauri hiyo.


Vaileth Ngesi ni mratibu wa ukimwi halmashauri ya mji wa Makambako,amesema kwa kuwa hali ya maambukizi bado inaendelea kupanda hivyo kwa kushirikiana na wadau itasaidia kupunguza kasi hiyo ya maambukizi


“Hali ya maambukizi bado inaendelea kupanda hivyo kwa kushirikiana na wadu mmbali mbali kama wenzetu wa Uwodo tunaamini kabisa maambukizi yataendelea kupungua tunawashukuru sana wenzetu wa Uwodo kwa kutufikia kwasababu pia wataweza kutoa elimu lishe kwa wasichana”alisema Vaileth Ngesi


Aidha wanaume 537 kati ya 10478 ambao walijitokeza kupima wamekutwa wakiwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi katika halmashauri ya mji makambako idadi yao ikiwa ni ndogo zaidi ukilinganisha na idadi ya wanawake waliobainika kuwa na maambukizi.


Jumla yao ni watu 1570 ambaowameripotiwa kukutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kipindi hicho cha miezi kumi huku sababu ya kuongezeka kwa maambukizi hayo ikitajwa kuwa ni mwingiliano wa watu wengi kibiashara kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nnje ya nchi.


Zaeli Ngigwa na Vashti Kifuso ni baadhi ya vijana wa kike na wa kiume wamesema vipo vishawishi vingi vinavyopelekea vijana kuingia kwenye ngono katika maeneo yao ikiwemo muingiliano wa wafanyabiashara pamoja na wasafirishaji wa mizigo huku wakiomba elimu iendelee kutolewa dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.


“Upo umuhimu wa kuendelea kutuelimisha watoto wa kike kujikinga na gonjwa la ukimwi kwasababu hapa Makambko kuna vishawishi vingi sana nah ii itatuepushia na maambukizi na hata wazazi wetu wamekuwa wakiendelea kutupatia elimu hata tunapokuwa tunaenda kwenye mahospitali”alisema Vashti Kifuso


Zaeli Ngigwa alisema “kuna umuhimu sana kutoa elimu na wazazi ifike mahala waelimishe wattoto bila woga juu ya janga la ukimwi na ninashauli tuendelee kujihadhari huku mabinti wajitahidi kubadirika hata kwenye mavazi”alisema Zaeli Ngigwa


Mkurugenzi wa Shirika la UWODO bwana Hamis Hasan Kassapa ambao wamechukua jukumu la kuelimisha vijana wa kike kuanzia miaka kumi na minne hadi ishirini na mitano,amesema mradi huo unatarajia kutekelezwa katika kata tatu za mji wa Makambako kwa muda wa mwaka mmoja mpaka Disemba 2021 ukiwa umefadhiliwa na ubalozi wa Marekani kupitia mfuko wa Rais PEPFA


“Tuko hapa kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wetu  wa uhamasishaji kwa wasichana kushiriki katika upimaji wa virusi vya ukimwi mradi utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja kwenye kata za Mji mwema,Mwembe togwa pamoja na Ubena”alisema Kasapa


Aliongeza kuwa “Tutafanya kazi na wasichana kwasababu hapa pana makutano na kuna magari yanayokwenda nchi za jirani na kuna wakati madereva wanapumzika hapa huku wengine wakiwatumia wasichana na tumeona wasichana wako kwenye hatari kunwa sana ya kushawishiwa na hatimaye kuingia kwenye ngono huku wengine wakiambukizwa na VVU”alisema Kasapa


Mji wa Makambako wenye msongamano wa watu kutokana na biashara pamoja usafirishaji wa mizigo kuelekea mikoa inayopakana na nchi jirani upo ndani ya mkoa wa Njombe ambao unatajwa kuongoza kitaifa kwa idadi kubwa ya maambukizi ya vvu kwa asilimia 11.4 ukifatiwa na mkoa Jirani wa Iringa.

Post a Comment

0 Comments