TANGAZA NASI

header ads

Mbunge Swale akataa ukanda,ataka maendeleo Lupembe

 



Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mbunge wa jimbo la Lupembe halmashauri ya wilaya ya Njombe Wakili Edwin Swale,amewaagiza madiwani wa halmashauri hiyo kujielekeza katika kujadili maswala ya maendeleo na shida za wananchi badala ya kujadili ukanda hatua itakayopelekea kurudisha nyuma jitihada za maendeleo ya halmashauri.


Swale amewaagiza madiwani wakati akitoa salamu zake katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mtwango wilayani humo kilichoambatana na zoezi la kuwaapisha madiwani.


“Tunapojadili maswala ya maendeleo tusijadili maswala ya ukanda,tuzungumze shida za wananchi wa jimbo la Lupembe kwasababu tukienda hivyo hatuwezi kujenga”alisema Mbunge Swale


Aliongeza kuwa “Kwa mapato ya ndani ya halmashauri,hata kama tungepata bilioni tano hatuwezi kupeleka miradi sawa kwa awamu moja kwenye kata zote ni lazima kuna kata fulani itapata zaidi kwa awamu ya kwanza ila jambo la msingi isipate zaidi mara mbili hilo lazima tukubaliane kwasababu keki ya taifa ni ndogo twende kwa awamu”alisema Swale


Vile vile ametoa rai kwa madiwani kuwa wamoja katika kusukuma maendeleo huku akiahidi kuto kuwa sambamba na mtu atakayekwenda kinyume na swala lenye maslahi ya umma.


“Itakapotokea wenzetu kati yetu,hatuendi kwenye njia moja ya kupeleka mbele halmashauri,kutofautiana itakuwa ni kawaida na mimi mbunge sitakuwa muoga kutofautiana na yeyote kwenye jambo linalohusu maslahi ya umma,huo ndio msimamo wa Rais na ni msimamo wa serikali ya Chama cha Mapinduzi”alisema Swale


Aidha amemuomba mkurugenzi kurekebisha bara bara ya Lunguya kwenda Welela kwa kuwa bara bara hiyo imekuwa na mchango mkubwa wakati wa usafirishaji wa mchanga kwenda maeneo mbali mbali unaotumika kwenye ujenzi.


“Wakati wa kampeni nimepita hili jimbo zima lakini kati ya barabara ambazo ni mbaya na inatoa mchango mkubwa kubeba mchanga ni bara bara ya Lunguya Kwenda Welela natamani mkurugenzi upite pale”alisema Swale


Kutokana na ombi hilo naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Ally Juma amemuahidi mbunge kushugulikia bara bara hiyo mapema iwezekanavyo huku akiwaeleza madiwani hao mpango wa halmashauri hapo baadaye kumiliki Gleda litakaloweza kusaidia katika urekebishaji wa barabara kwa wakati na kuisaidia Tarula


Ruth Msafiri ni mkuu wa wilaya ya Njombe,kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewaomba madiwani kusahau tofauti zao na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya halmashauri.


“Tusithubutu kufanya yale ambayo hayasaidii kwa sasa,tuhakikishe tunashirikiana kwa nguvu na kwa pamoja huku tukisahau tofauti zetu.Ilani ya Chama  cha Mapinduzi na hotuba ya Mh,Rais view ni dira ya utendaji wa baraza hili”alisema Ruth Msafiri

Post a Comment

0 Comments