TANGAZA NASI

header ads

MKUU WA WILAYA NYASA AWATAKA WAKULIMA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO LA KAHAWA



 Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba, amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuongeza Uzalishaji wa zao la kahawa kwa kulima mbegu za kisasa, zinazozalisha mazao bora ya kahawa ili kukuza uchumi wa kaya na mapato ya wilaya kwa ujumla.

Ameyasema hayo hivi karibuni, alipofanya ziara ya siku moja katika Kata ya Upolo na Luhangarasi katika Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa, Ziara yenye lengo la Kufunga mafunzo ya Mgambo katika kata ya Upolo, kuhamasisha kilimo cha Kahawa na kuhamasisha jamii kuandaa majengo na madawati kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza Wilayani hapa.

Chilumba amefafanua kuwa Wilaya ya Nyasa ina mashamba makubwa ya kuweza kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa, ukilinganisha na Wilaya ya Mbinga ambayo kwa sasa ni wazalishaji wakubwa wa zao la kahawa, hivyo amewataka wakulima wa zao la kahawa hasa katika Tarafa za Mpepo ambao ndio wazalishaji wakubwa wa zao hilo kulima mbegu bora kwa kuongeza mashamba mapya ya kahawa.

Serikali imegawa bure miche 7000 katika Wilaya ya Nyasa, kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa Hivyo amewaagiza viongozi wa kata.vijiji na vitongoji kuhakikisha miche hiyo inapandwa na uzalishaji unaongezeka.

Kwa upande wa uhamasishaji wa kuandaa majengo na madawati kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2021 Mkuu huyo amewataka wananchi na viongozi ngazi ya kata kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anaripoti shuleni na kuwaagiza atachukua hatua za kisheria kwa mzazi au mwanafunzi atakayeshindwa kuripoti Shuleni.

Katika Kata ya Upolo Wilayani hapa alifunga mafunzo ya Mgambo ambayo amewataka wahitimu kuyatumia mafunzo hayo katika kulinda usalama wa Nchi na kutoruhusu wageni kuingi bila kibali ukizingatia kuwa tumepakana na Nchi ya Msumbiji.

Aidha mewataka mafunzo waliyoyapata kutumia kuzalisha Zao la kahawa na  kuhamasisha jamii waweze kujiongezea kipato katika uzalishaji mali na kukuza mapato ngazi ya kaya na Hlmashauri kwa ujumla

Post a Comment

0 Comments