SALVATORY NTANDU
Jumuiya
ya kiislamu ya International Istiqaama muslim Community imetoa
msaada ya vyakula mbalimbali kwa Wafungwa waliofunga katika Gereza la
wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ili kuwasaidia katika kipindi hiki cha
mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akikabidhi
Msaada huo Mei 9 mwaka 2020 kwa mkuu wa Gereza hilo, Misana Shigumha
Katibu wa Masijd Alwahab kahama, Shekhe Ahmed Haroun Alnoobiy
amesema msaada huo umetolewa na watu kutoka taifa la Oman kwaajili ya
wafungwa na kuwataka kuendelea kuwaombea ili mwenyezi mungu aendelee
kuwapa kheri zaidi.
“Tumeleta
kilo 200 za mchele, kilo 200 maharage ndoo saba za mafuta ya kula, na
sukari kilo 100,tunaomba mpokee,ndugu zenu wa oman wamewakumbuka kwa
msaada huu naombeni muendeleze dua katika kipindi hiki cha toba,”alisema
Alnobiy.
Aliongeza
kuwa Jumuiya hiyo hapa nchini inahusika na kuisaidia jamii hususani
yatima, masikini na wagonjwa ndio maana ikaamua kuwasaidia wafungwa hao
ili nao waweze kumrudia Mwenyezi Mungu kwa kufanya toba katika kipindi
hiki maalumu cha mwezi Mtukufu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Masijd Alwahab Kahama, Shekhe Mohamed Issa
amewaomba wafungwa kuutumia mfungo huu wa Mwezi wa Ramadhani kwa
kumwombea Rais, Dk John Pombe Magufuli ili Mwenyezi Mungu aendelea kumpa
hekima za kuliongoza taifa kwa amani.
“Dumisheni
dua ili Mwenyezi Mungu aweze kutuondelea janga la Corona ambalo
linaendelea kuutikisa ulimwengu,tunaimani Allah atatukinga na kutuepusha
dhidi ya COVID 19,”alisema Issa.
Akipokea
Msaada huo kwa niaba ya Kamishana Jenerali wa Jeshi la Mageraza
nchini,Mkuu wa Gereza hilo,Misana Shigumha ameishukuru jumuiya hiyo kwa
msaada huo na kusema kuwa utawafikia wafungwa hao kwa wakati.
Sambamba
na hilo Misana amesema kuwa katika jitihada ka kukabiliana na ugonjwa
homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona katika gereza
hilo wanaendelea kuzngatia maelekezo yote yaliyotolewa na serikali ikiwa
ni pamoja na kuzingatia unawaji wa mikono na upimaji wa joto kwa
wafungwa,mahabusu na watu wengine wanaotembelea eneo hilo.
0 Comments