TANGAZA NASI

header ads

"NITAHAKIKISHA JENGO HILI LINAKAMILIKA KWA MUDA MFUPI" MBUNGE JASON RWEIKIZA BUKOBA VIJIJINI




Na Theophilida Felician Kagera.

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mhe  Dkt Jason Rweikiza amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Kabirizi Kata ya Kaibanja   Bukoba Vijijini Mkoani Kagera kuwa jengo linalojegwa kijijini hapo la kutolea huduma ya mama na mtoto linakamilika upesi nakuanza kuwahudumia wananchi wa kijiji hicho wanaopata adha kuipata kwa usahihi huduma hiyo kwa sasa.

Dkt Rweikiza ameyaeleza hayo mbele ya wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo linakojengwa jengo hilo alipokuwa amefika kukagua maendeleo ya ujenzi wake pamoja na kutoa shukran kwa wananchi hao kwa jinsi walivyomchangua kwa kura zakishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

"Sasa ndugu zanguni tulikoanzia katika ujenzi wa Kliniki hii ni mbali mno ila ona tumebakisha hatua chache tuu ili tukamilishe ujenzi huu mimi kama mbunge wenu nitafanya juu chini na kuhakikisha naongezea nguvu ya kiasi cha Sh Milioni 5 mulioisema kuwa inakosekana ili ziweze kusaidia ukamilishaji wa jengo letu na tuanze kuhudumiwa sehemu nzuri na imara nimependezeshwa na ubora wa ujenzi wake hongereni sana mumenitia moyo zaidi nasema likiisha liwekewe umeme, maji na huduma nyingine  muhimu ndo maendeleo hayo tunayoyapigania kila siku" alisema kwakina mbele ya wananchi hao Mbunge huyo huku akimuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri afanye jitahada katka utafutaji wa pesa nazo zisaidie kuyakamilisha mahitaji yatakayokuwa bado yanahitajika katika kulikamilisha jengo hilo.

Mbunge huyo vilevile ameyafikia maeneo mbalimbali zikiwemo kata za Kibirizi, na hiyo ya  Kaibanja, Izimbya, Kishogo na nyinginezo, na huko nako aliendelea kuunga mkono juhudi za wananchi kwakuchangia michango zaidi katika ujenzi wa majengo hususani ya yale yakutolea huduma za mama na mtoto hasa kwa yale maeneo ambako huduma hiyo imekuwa shida kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kazinga Firbet Ntom amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia hatua ya mwisho na tayari zimeishatumika zaidi ya  Milioni 71 kutoka sehemu tofauti tofauti  ikiwemo ya Sh Milioni 15 iliyotolewa na Mhe Mbunge  hivyo kiasi hicho atakachokiongezea Mhe Mbunge tena pamoja na michango ya wananchi sambamba na ya Serikali kitakamilisha ujenzi huu kwani mahitaji yaliyobakia ni machache yakiwemo ya sakafu, ujenzi wa vyoo, benchi zakukalia nk, na kwa hali hiyo  "wananchi wa Kazinga tunamshukuru sana mbunge make mikakati na mipango ya suala la ujenzi wajengo kama hili  ni la zamani  sana wamepita viongozi wengi ilishindikana kupatiwa ufumbuzi ila chini ya Mhe Rweikiza Neema imeshushwa na tayari tunaelekea  kuitimiza ndoto yetu tunajivunia uwepo wake tunatamani atuongoze daima akina mama wamehangaika sana tumejenga majengo ya muda lakini wapi shida zimeendelea kutuandama kila wakati" maneno ya  mwenyekiti  mbele ya Kiongozi huyo.

Kwingineko Dkt Jason alikowafikia wananchi nao wakiwemo hao wa Kijiji cha Kazinga walizidi kutoa shukrani zao kwa Mbunge huyo kwa jitihada alizonazo juu ya kujinyima na kuyapigania maendeleo yao huku wakizidi kumuomba aendelee kuwasaidia kuwaunga mkono pale panapowezekana hasahasa katika ukamilishaji wa miradi mbalimbali iliyoanzishwa katika maeneo yao.

Post a Comment

0 Comments