TANGAZA NASI

header ads

JAMII YATAKIWA KUWA NA USHIRIKIANO KATIKA MALEZI




NA THABIT MADAI, ZANZIBAR

MKURUGENZI Mtendaji Tume ya Kitaifa ya kuratibu na Udhibiti wa dawa za kulevya Zanzibar Luteni Kanal Burhani  Zuberi Nassor ameitaka  jamii kuwa na mashirikiano katika  malezi ya watoto ili kuepuka kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Ameyasema hayo huko katika ukumbi wa Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais katika ukumbi wa Migombani wakati alipokuwa akizungumza na  waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya madawa ya kulevya ambayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 26 mwezi huu huko katika ukumbi wa shekh Idriss Abdulwakil ambapo mgeni rasmi Rais wa ZanzibarDkt Hussein Ali Mwinyi.

A mesema dawa za madawa ya kulevya hivi sasa ni tishio Zanzibar ambapo vijana ambao ndio nguvu kazi kwa taifa wamekuwa ndio waathirika wakubwa wa kutumia madawa hayo na kuahidi kujipanga ili kuondoka kabisa kupitia vikosi vyote vya ulinzi na usalama.

Hivyo amesema tuwe na mashirikiano katika kuwa nao karibu watoto  na iwapo unamuona na kitu ambacho kiko nje ya uwezo wake kifatiliwe ili kumnusuru na janga hilo kwani tusipokuwa imara  wazazi basi baada ya miaka 20 kila nyumba moja itakuwa na mteja.

Pia ameitaka jamii kuondoa muhali kwa kulindana mitaani na kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwa kila anayeuza biashara hiyo ili tuweze kupunguza kadhia hiyo ambayo imekuwa kila sehemu katika mitaa yetu.

Aidha amesema zaidi ya watu elfu kumi wameathirika na madawa ya kulevya na kuitaka jamii ibadilike ili kuokoa kizazi chetu kisizidi kuteketea.

Nae Mkurugenzi wa Udhibiti na Uchukuzi Juma  A. Zidikheiry amesema ripoti za kitengo cha Polisi cha kupambana na dawa za kulevya zimeonesha katika kipindi cha miaka 9 iliyopita 2012-2020 jumla ya watuhumiwa 3,810 wakiwemo wanaume3,577 na wanawake 233 wamekamatwa nchini wakijihusisha na uhalifu wa dawa za kulevya .

Hata hivyo amesema katika kipindi hicho jumla ya kilo 51.5 za heroini kilo 2,946 za bangi . kilo 5.4 za valiamu na kilo 19.71 za kokeni zilikamatwa.

Zanzibar bila ya madawa ya kulevya inawezekana  ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni sema ukweli juu ya athari ya madawa ya kulevya okoa maisha .

 

Post a Comment

0 Comments