TANGAZA NASI

header ads

Halmashauri ya mji Makambako yapokea mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule

 


Na Clief Mlelwa,Makambako


Halmashauri ya mji wa Makambako imepokea mifuko 40 ya saruji yenye thamani ya shilingi laki sita na elfu themanini kutoka kwa wamiliki wa vituo vya kulele watoto wadogo Day care center).

Wakikabidhi mifuko hiyo wamiliki wa vituo hivyo wamesema Kuwa mifuko hiyo ya saruji imetolewa ili kuboresha miundombinu mbalimbali kwenye shule za msingi katika halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako Paulo Malala amesema kuwa shule nne zitaenda Kunufaika na saruji hiyo ikiwemo shule shikizi ya maguvani,shule ya Msingi kwauchungu,Maendeleo na Mfumbi,ambapo kila shule itapata mifuko kumi.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya mji huo,Hanana Mfikwa amesema kuwa vituo vya kulelea watoto wadogo vimekua na msaada mkubwa katika kupunguza matukio ya ukatili kwa watoto na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za Msingi.

Kwa mwaka huu wa 2021 jumla ya watoto wadogo 2065 wamesajiliwa katika vituo hivyo.

Post a Comment

0 Comments