Mkurugenzi
wa wilaya ya Makete Francis Namaumbo akizungumza na wachungaji pamoja baadhi ya
waumini wa kanisa la KKKT Makete mjini wakati akizindua mpango maalum wa kanisa
hilo kufika vijijini kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.
Askofu
wa KKKT Jimbo la Kusini kati akizungumza na waumini kabla ya uzinduzi wa elimu
dhidi ya virusi vya Corona.
Afisa
afya wilaya ya Makete BONIFASI SANGA akitoa elimu na kutoa pongezi kwa Mkanisa kuona
umuhimu wa kuisadia serikali katika mapambano ya Corona.
Baadhi
ya washonaji wa Barakoa kutoka kituo cha Udiakonia Tandala ambao ni walemavu wa
viungo wakiwa katika eneo lao maalum la kushona Barakoa.
Baadhi
ya waumini waliofika kanisa la KKKT Makete mjini pamoja na wachungaji
wakishudia zoezi la uzinduaji mpango maalum wa kufikisha elimu dhidi ya virusi
vya Corona vijijini wilayani Makete.
Na
Amiri kilagalila,Njombe
Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini Kati wilayani Makete
mkoani Njombe,kwa kushirikiana na Madhehebu mengine wilayani humo,wamezindua
mpango Maalum wa kudhibiti na kupambana na virusi vya Corona (COVID-19) na
kufika kila kijiji ndani ya wilaya ili kutoa elimu ya kupambana na kirusi
Corona.
Askofu
wa Dayosisi ya Kusini kati Wilson Sanga amesema tangu tatizo hilo lilipoingia
nchini,Kanisa limeungana na serikali kuunga mkono juhudi za Serikali katika
vita dhidi ya Corona.
“Tangu
tatizo hili lilipoingia kanisa la Kilutheri pamoja na vyama vya wamisioni Ulaya
na Amerika,Jumuiya ya Kikristo Tanzania vyote vimeungana na serikali kuunga
mkono katika vita dhidi ya Corona,hii ikiwa ni pamoja na baadhi ya vyama kutoa
fedha au kuruhusu fedha ambayo Dayosisi ilipanga kutumia kwa miradi maalum
kwamba sasa fedha hiyo inaweza ikatumika katika mpango wa kupambana na virusi
vya Corona.Hivyo Dayosisi imeamua kunzisha mpango huu ambao katika hatua za
awali unakadiliwa kutumia kiasi cha Milioni 15”alisema Askofu Wilson Sanga
Akizungumza
kwa niaba ya mganga mkuu wa wilaya ya Makete,Bonifas Sanga ambaye ni afisa afya
wa wilaya,amesema awali kabla ya kuruhusu kanisa kuanza mpango huo,serikali
kupitia idara ya afya imefanikiwa kudhibitisha ubora zikiwemo Barakoa na vifaa
vingine vitakavyotumika wakati wa uelimishaji vijijini pamoja na kugawa kwa
makundi maalum.
“Nipende
kupongeza kwenye maeneo ambayo mnaanza kuhudumia hapa Makete wakiwemo Walemavu
na wazee,na nitamke hapa kwamba vifaa vya barakoa vilivyoandaliwa na kundi hili
vina ubora na vinaruhusiwa kutumika”alisema Bonifasi Sanga
Ronester
Mgaya na Hekima Mgenzi ni baadhi ya walemavu wanaofanya shughuli za ushonaji wa
Barakoa zilizokidhi vigezo katika kituo cha Udiakonia Tandala na kukubaliwa na
wataalamu wa Afya Makete.Wameishukuru Dayosisi pamoja na serikali kuona umuhimu
wa kuinusuru jamii ya Makete dhidi ya Corona.
Akizundua
mpango huo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Francis Namaumbo kwa
niaba ya mkuu wa wilaya.Amesema serikali serikali ya wilaya imeunda timu
zinazotembea na kufuatilia kuhakikisha wananchi wananchi wanaendelea kufuata
maelekezo huku akipongeza mpango huo wa kanisa.
“Kwa
hiyo nanyi tuendelee kutoa maelekezo dhidi ya corona katika nyumba zetu na
familia zetu na kila familia ikichukua tahadhari kwa asilimia mia tutakuwa
salama”alisema Namaumbo
Aidha
amewaasa wana Makete kufanya ajenda ya kupambana na virusi vya Corona kuwa ya
Kudumu ili virusi visweze kuenea wilayani humo.
0 Comments