Na Jackline Kuwanda,Dodoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa
na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka madaktari wapya 610
walioajiriwa chini ya mamlaka za mitaa hivi karibuni kuhakikisha ndani ya
wiki mbili kuanzia mei 11 mwaka huu wanaripoti katika maeneo
waliyopangiwa.
Kuajiriwa kwa madaktari hao kunafanya
idadi ya madaktari walioajiriwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie
madarakani chini ya Rais Dkt John Magufuli kufikia 9,839 katika mamlaka za
serikali za mitaa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
ofisini kwake jijini Dodoma Jafo amesema madaktari hao wamepangiwa katika vituo
vya Afya,Zahanati na Hospitali za wilaya.
Ametoa maagizo kwa madaktari hao
ikiwemo kwenda kuongeza weledi kwenye maeneo yao katika kupambana na virusi vinavyosababisha
ugonjwa wa homa kali ya mapafu(COVID 19) na pia kuhakikisha wanaripoti wakiwa
na vyeti vyao vya taaluma.
Februari
20 Rais Magufuli akifungua mkutano wa 55 wa Chama Cha Madaktari Tanzania(MAT)na
watumishi wa sekta ya afya uliofanyika katikaukumbi wa kimataifa wa mikutano wa
Julius Nyerere(JNICC)alitangaza kuajiri madaktari 1,000.
Mwezi
mmoja baadae TAMISEMI ilitangaza ajira hizo 610 na kuwataka waombaji waombe
kuanzia Machi 24 hadi April 10 ambapo zoezi hilo lilifungwa.
0 Comments