Na Ibrahim
Mlele,Njombe
Zaidi
wananchi 2700 kijiji cha Havanga halmshauri ya wilaya ya Njombe wameanza
kunufaika na mradi wa umeme uliobuniwa na Frank Kihombo mkazi wa kijiji cha Nyombo
baada ya kuikosa nishati hiyo kwa muda mrefu.
Wakizungumza na kituo hiki kijijini hapo wananchi hao wameshukuru mbunifu huyo kwa kujitokeza kuanzisha mradi huo ambao unawasaidia katika matumizi mbalimbali ikiwemo kupata mwanga na kupata taarifa kupitia televisheni na radio.
“Tunanufaika kwa mambo
mengi sana kupitia huu umeme mfano mimi ni fundi simu kuna baadhi ya vitu
tulikuwa hatuvitumii kulingana na umeme haukuwepo lakini safari hii tunavitumia
kwasababu umeme upo”alisema Alex Kapinga
moja ya mwananchi fundi umeme kijijini hapo
Mbunifu huyu anasema hana taaluma ya ufundi wa umeme ila amekuwa na kipaji tangu alipozaliwa na alihamasika kuanzisha mradi katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wanataabika ingawa mradi huo bado haujakamilika kutokana na kukosa vifaa mhimu zikiwemo nyaya.
“Nilipofika hapa
nikakutana na maji ya kutosha na wananchi wanaishi kwa kutumia solar,jua lisipowaka
hawana mwanga nikaona wacha niwasaidie nitengeneze huu umeme ili waweze kupata nuru” Frank Kihombo
“Niliona
nitengeneze huu umeme watu wapate nuru wakati huo nikionesha kipaji change kwamba
ndoto zilizokuwa zinanitesa nionekane nilisaidia watu”aliongeza Frank Kihombo
Vile vile ameomba
serikali kupitia shirika la umeme Tanesco kumsaidia miundombinu
“Ninaomba wanisaidie
miundombinu ambayoninakosa kwa mfano waya,nguzo baadhi ya mitambo ninayo transfoma
za kusuka ninaweza za ukubwa wowote ule lakini kuna vifaa vingine sina uwezo
navyo na pesa kwa sasa sina” Frank Kihombo
Serikali ya kijiji cha Havanga kupitia mtendaji wake Philimoni Lulimo imesema iliitisha kikao baada ya mbunifu huyo kujitokeza katika kuanzisha mradi na wameshirikiana naye kwenye baadhi ya shughuli na kwamba mradi huo umekuwa ni sehemu ya kuchochea maendeleo.
“Sasa hivi umeme huu unasaidia kwa maana ya matumizi
ya kawaida majumbani na kwenye taasisi watoto wetu wa shule ya msingi wanapata
neema ya kusoma hata usiku bila ya kuwa na kikwazo” alisema Philimoni Lulimo
Miezi
kadhaa iliyopita kadhalika mkoa Njombe ulifanikiwa kuibuliwa wabunifu watatu
kutoka vijiji tofauti hali iliyopelekea Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt,John Pombe Magufuli kuagiza wataalamu mbali mbali wakiwemo kutoka Tanesco
kuwasaidia wabunifu hao kutokana na huduma wanazotoa kwa jamii.
0 Comments