TANGAZA NASI

header ads

Shule ya msingi Kitewele wilayani Ludewa mkoani Njombe yakabiliwa na utoro uliokithiri



Na Joctan Myefu,Njombe

Shule ya msingi Kitewele iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe inakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya elimu na kusababisha wanafunzi kutohudhuria vipindi na utoro uliokithiri na kupelekea shule hiyo kuathirika kitaaluma kwa kiasi kikubwa.

Shule ya Kitewele iliyopo kata ya Mawengi inakabiliwa na adha kubwa ya upungufu wa madarasa,Maktaba,walimu pamoja na nyumba za kuishi watumishi jambo  ambalo limesababisha watoto wengi kutopenda kwenda shule na kuamua kujikita katika uvuvi,kilimo na ufugaji.

Wakizungumzia changamoto zinazokwamisha maendeleo ya taaluma katika shule hiyo January Ngailo ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kitewele na Agustino Mkamanga mtendaji wa kijiji cha Kitewele wanasema changamoto hiyo imetokana miundombinu isiyorafiki ya elimu.

Sypria Ally na Kulaini Mwinuka ni baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kitewele ambao wanasema wamekuwa wakisoma  katika mazingira magumu hususani katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa corona hivyo serikali na wadau waone namna ya kuboresha mazingira ili kufanya vizuri kitaaluma  

Kufuatia kilio hicho cha muda mrefu ndiyo mratibu wa mradi wa kusaidia elimu wa MAMMIE unaotekelezwa na shirika la shipo kwa ufadhiri wa WE WORLD Nemes Temba wakati akitoa elimu ya Corona pamoja na msaada wa vifaa vya kinga vya ugonjwa wa corona anasema amelazimika kufika na kujionea hali ilivyo katika shule hiyo na kuahidi kuendelea kusaidia kuzitafutia majibu changamoto hizo ikiwemo ya nyumba za walimu na madarasa.

Zaidi ya shule 20 ikiwemo Kitewele zimejengewa miundombinu ya maji ili kukabiliana na corona. 

Post a Comment

0 Comments