Leo Julai 7, 2020, mwanachama wa CHADEMA Dkt Mayrose Majinge, amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.
Dk. Majinge amekabidhiwa fomu hiyo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Reginald Munisi, katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo , Dk. Majinge ametaja mambo kadhaa ambayo atayafanyia kazi endapo atachaguliwa na Chadema kugombea nafasi hiyo na kisha kupata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa Tanzania.
Dk. Majinge amesema, endapo atapata ridhaa hiyo, atajenga mfumo imara na madhubuti wa uongozi wa taifa, kwa ajili ya maslahi ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Amesema ahadi yake kwa Watanzania ni kuwezesha upatikanaji wa katiba ya wananchi na tume huru ya uchaguzi
0 Comments