INAELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato wa kusaka saini ya kiungo Fabrice Mugheni, raia wa DR Congo.
Mugheni
ni miongoni mwa viungo bora katika Ligi Kuu ya Rwanda na aliwahi
kuletwa nchini na aliyekuwa kocha wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma lakini
viongozi wa timu hiyo hawakuridhishwa na uwezo wake aliouonyesha katika
majaribio yake kama ilivyokuwa kwa Mghana, Lamine Moro kabla ya kutua
Yanga.
Wakati
anatua kwa mara ya kwanza, kiungo huyo mwenye uwezo wa kupiga mashuti
ya mbali, alifichwa na viongozi wa Simba ikiwemo kumbadilishia ndege ili
kukwepa kuonekana na hata alipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA), alitolewa kwa usiri mkubwa majira ya saa nane
usiku huku akiwa ameziba sura na kukimbizwa haraka kwenye gari iliyokuwa
ikimsubiri lakini Championi lilimnasa akipokelewa na Mratibu wa Simba,
Abbas Ally.
Taarifa
za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa tayari Mkurugenzi wa
Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Mhandisi, Hersi Said tayari ameshakamilisha
mazungumzo na kiungo huyo na kinachosubiriwa ni kuweza kusaini mkataba
tu.
“Unajua
usajili wa Sarpong hauwezi kuwa mgumu kwa sababu mkataba wake umevunjwa
na Rayon lakini kuna kiungo mwengine yupo pale tayari uongozi unafanya
mipango ya kumleta na mchezaji ameonyesha utayari wa kuja kwani mkataba
wake unaelekea kuisha.
“Ni
yule jamaa mwenye rasta anaitwa Fabrice aliwahi kuja Simba akafanya
majaribio lakini wakamkaushia ila mhandisi Hersi ameshamalizana naye na
kinachosubiriwa ni hili janga la Corona lipite,” alisema mtoa taarifa.
Championi
lilimtafuta kiungo huyo ili aweze kuzungumzia ishu hiyo ambapo alisema:
“Ni kweli nimefuatwa na viongozi wa Yanga lakini siwezi kusema nini
nimezungumza,".
(Salehe jembe)
0 Comments