KIUNGO
mshambuliaji wa Simba, Hassan Dilunga, amesema kuwa kwa sasa hafikirii
kurejea tena Yanga na akili zake amezielekeza kucheza soka la kulipwa
nje ya nchi.
Dilunga
ni kati ya wachezaji waliowahi kucheza Yanga na sasa yuko Simba ambako
mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu
Bara.
Kiungo
huyo hivi karibuni alikuwa akitajwa kuwaniwa vikali na Yanga ambayo
inaelezwa alitengewa dau la Sh Mil 80 ili asaini mkataba wa miaka miwili
ya kukipiga Jangwani.
Dilunga
amesema kuwa ndoto zake zimefanikiwa za yeye kucheza kwenye klabu kubwa
hapa nchini za Simba na Yanga, alichobakisha yeye ni kucheza nje ya
nchi.
“Ndoto
za wachezaji wengi hapa nchini ni kucheza klabu kubwa za Simba na Yanga
ambazo mimi pia ilikuwa ndoto zangu ambazo zimefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kwangu.
“Nimepata
taarifa za mimi kutakiwa na timu yangu ya zamani ya Yanga, nilikuwa
tayari kurejea huko lakini kwa hivi sasa sitakuwa katika sehemu nzuri ya
kurejea huko.
“Ninataka
kutimiza malengo yangu ya mimi kucheza nje ya nchi na huu ninaamini
ndiyo wakati wangu muafaka wa kwenda huko kucheza kama siyo nchi za
Ulaya basi Afrika,” amesema Dilunga.
Chanzo: Championi
0 Comments