Taarifa
zinaeleza kuwa Ligi Kuu ya England inaweza kurejea Juni 8 ambapo
kutakuwa na maandalizi mafupi ya muda wa wiki tatu kwa timu shiriki na
wachezaji pia watawekwa karantini kabla ya kuanza kucheza. Nyota
wa timu ya Manchester United wameambiwa kuwa wanatakiwa kuanza
kujifulia nguo zao wenyewe kuelekea kurejea kwa mazoezi Mei 18. United inajiaandaa kurejea kwenye mazoezi baada ya Ligi Kuu ya England kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona. Wachezaji
wa United pia wanatakiwa kutumia usafiri binafsi wanapokwenda mazoezini
Uwanja wa Carrington na wanatakiwa kuoga kwenye mabafu ya nyumbani
kwao. Maamuzi
ya kutakiwa kuosha na kufua vifaa vyao vya mazoezini ni kwa sababu
hakutakuwa na huduma hiyo kwa kipindi cha hivi karibuni na wale
wachezaji waliosafiri nje ya England kujitenga Siku 14 pale
watakaporejea ili kuona kama wana maambukizi ya Corona. Manchester
United ipo nafasi tano Kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 45 kibindoni
baada ya kucheza mechi 29 na kinara ni Liverpool mwenye pointi 82 baada
ya kucheza mechi 29. (Salehe jembe)
0 Comments