Na Said Mwishehe BALOZI
wa Tanzania nchini Uingereza Dk.Asha-Rose Migiro amesema katika
kukabiliana na virusi vya Corona hata huko waliko nako wanapiga
Nyungu(kujifukiza) kama kawaida maana kila mtu anatafuta namna ya
kujiokoa.
Dk.Migiro amesema hayo leo Mei 11 mwaka 2020 na
kufafanua licha ya kwamba yeye na Watanzania wengine kuwepo Uingireza
ukweli wanatambua nyungu ni kitu cha asili na huko wanapiga nyungu sana
tu."Unajua kila mtu anatafuta njia mbalimbali za kujiokoa."
Akifafanua
zaidi wakati anahojiwa na kipindi cha 360 kilichorushwa na Clouds
Media,Balozi Dk.Migiro amesema pia anatambua jitihada mbalimbali ambazo
zinafanywa na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika kutafuta dawa ya
kukabiliana na Corona.
"Kuna hatua ambazo zinaendelea kwa nchi za
Afrika, kama ambavyo tunafahamu kwa sasa Corona haina dawa wa kinga,
hivyo kila nchi inajaribu kuangalia namna ya kusaidia wananchi wenye
kwenye janga hili.Hata dawa ya Madagasca napongeza Rais Dk.John Magufuli
alivyoamua kutuma ndege kwa ajili ya kuifuata dawa hiyo.
"Tunafahamu
mataifa yote yanahaha kutafuta dawa na hadi sasa hakuna dawa ambayo
imethibika kisayansi kuwa inatibu Corona, hivyo dawa ambayo itapatikana
kwa sasa basi hiyo hiyo itatumika, maana hata unapozuia watu wasinywe,
kuna tiba ipi nyingine mbadaka ambayo unampa atumie.Hivyo dawa ambayo
imetolewa na Madagasca kwa Tanzania ni hatua nzuri.
"Na nimeona
kupitia mitandao kwetu hapo nyumbani Tanzania kuna jitihada ambazo
zinafanyika kupata dawa na nimeona kuna dawa imeonekana kuwa na uwezo wa
kutibu Corona.Ni hatua nzuri kwa nchi za Afrika katika kupambana na
ugonjwa huu,"amesema Dk.Migiro.
Kuhusu uwepo wa Tanzania nchini
Uingereza wenye kupatwa na maambukizi ya Corona, Balozi Dk.Migiro
amesema kwa taarifa ambazo wanazo idadi ya waliopatwa na maambukizi ni
Watanzania kati ya 15 na 20.
"Ukweli wapo Watanzania ambao
walipatwa na maambukizi ya Corona hapa Uingereza lakini wengi
wanaendelea vizuri tu na afya zao zimeendelea kuwa imara,"amesema
Dk.Migiro na kuongeza kuwa kwa sasa Uingereza ndio inayoongoza kwa Bara
la Ulaya kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha.
0 Comments