Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wananchi mkoani Njombe wameeleza kufurahishwa na
ujenzi wa barabara za Njombe -makete kwa kiwango cha lami na ile ya Nyigo -Igawa
zenye urefu wa takribani kilomita 171 na kugharimu mabilioni ya fedha ambazo ni
kodi za watanzania.
baadhi ya wakazi hao akiwemo Adebayo Salum na Zakayo
Mbwilo toka Moronga Njombe wanatoa kauli hiyo wakati wa ziara ya chama cha
mapinduzi CCM mkoa wa njombe kupitia ofisi ya siasa na uenezi ilipofanya
ukaguzi wa ujenzi wa barabara hizo ambao wamesema kwenda kukamilika kwa miradi
hiyo kutakuwa fursa kwao kwa kuwa kumekuwa na adha kubwa ya usafirishaji mizigo
wakati wa masika na hata gharama kubwa ya nauli kwenye mabasi.
“Barabara hii awali ilikuwa mbovu sana na ilkiuwa
haipitiki kifuku lakini pia mazao yalikuwa hayatoki vizuri na bei ilikuwa
ndogo,kwa hiyo sisi tunaishukuru sana serikali kwa kutuona”Alisema Adebayo Salum
Erasto Ngole ni katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa
wa Njombe wakati akikagua ujenzi wa barabara hizo amewataka wakazi wa Makete
kutumia barabara hizo kama fursa kwao katika kujiletea maendeleo na kutakiwa
kurudi kuwekeza sasa.
“Mwaka 2015 tuliwaahidi watanzania kwamba barabara
ya Njombe-Makete na baadaye barabara ya
Makete kuelekea Mbeya,mitambo mnayoiona ipo kazini na utekelezaji
unaendelea,tunategemea barabara hii ndani ya miezi mitatu iwe imekamilika”
alisema Erasto Ngole katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe
Ngole aliongeza tena
“Wana Njombe
na wana Makete tutumie fursa hii ya kupata barabara kutoka kwa Mh,Magufuli kwa
kufanya kazi zaidi kwa kuwa tunakwenda kuifungua wilaya ya Makete na sasa muda
Umefika kwa wanamakete kuja kuwekeza kwasababu miundombinu sasa ni rafiki” alisema
Erasto Ngole katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe
Akikagua matumizi ya barabara ya Nyigo- Igawa,kutoka
Makambako kuelekea mkoani Mbeya iliyoanza kutumika mara baada ya kuzinduliwa na
Rais Magufuli mwishoni mwa mwaka uliopita, yenye urefu wa kilomita 64.6 kwa
gharama zaidi ya shilingi bilioni 103 bwana Ngole amewataka wananchi kutunza
miundombinu hiyo huku akilitaka jeshi la polisi lenye wajibu wa kulinda raia na
mali zao kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika barabara hizo.
Barabara hizo zimetakiwa kutumika vyema na wakazi wa
mkoa wa njombe na mataifa mengine katika kuwaingizia uchumi na pato la taifa
kwa ujumla.
0 Comments