Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Katika kuadhimisha miaka
56 ya jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania hii leo Septemba 1,2019. Kikosi cha
514 Makambako kimetoa msaada wa vitu mbali mbali katika kituo cha kutibu watu
wenye ulemavu wa viungo cha Inuka wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Pamoja na
kuchangia damu katika kituo cha afya cha Jeshi mjini Makambako.
Meja Iddi Sechonge
kaimu kamanda kikosi cha jeshi la ulinzi wa wananchi kikosi cha 514
Makambako akikabidhi misaada hiyo katika kituo cha Inuka amesema kuwa jeshi
linaadhimisha kuanzishwa kwake kwa kutoa misaada katika jamii inayolizunguka
ili kuwasaidia wasiojiweza.
“Tunaadhimisha
kuanzishwa kwa jeshi letu,kwa maana tumeona tushehereke na kituo hiki kwa ajili
ya kuwapa chochote,lakini kuna wenzetu wanaendelea na zozi la kuchangia damu”alisema
Meja Iddi Sechonge
Kaimu mkurugenzi wa
kituo cha Inuka Dokta Salehe Abdalaha amesema kuwa jamii bado inaimani potofu
dhidhi ya watu wenye ulemavu Pamoja na kueleza kuwa misaada zaidi inahitajika
kwa kuwa baadhi yao hushindwa kumudu gharama za matibabu.
“Kuna changamoto ya
uelewa kwenye jamii na baadhi yaw engine wanadhaani ni laana lakini sisi tunachosema
mtu anaweza akapata uleamvu saa yoyote”alisema Dokta Salehe Abdalaha
Zaidi ya uniti 35 za
damu zimepatikatikana katika kituo cha afya cha jeshi la ulinzi wa wananchi
kikosi 514 Makambako Mkoani Njombe
0 Comments