Na Amiri Kilagalila’Njombe
Kituo cha afya Mlangali wilayani Ludewa mkoani
Njombe kimefanikiwa kuanza kupokea karibu wajawazito 50 kutoka 15 wa awali kwa
mwezi,kutokana na kuimarishwa kwa huduma za afya na uboreshaji wa majengo
uliofanywa na serikali ya awamu ya tano.
Mganga mkuu wa kituo hicho cha afya kata ya Mlangali
Dkt,Rebeca Mduma amewaeleza waandishi wa habari kuwa awali kituo kilikuwa
kikipokea wajawazito wachache kutokana na akina mama wanaohitaji kupata huduma
kuelekea katika vituo vingine vinavyotoa huduma zinazokidhi mahitaji ya
wajawazito.
“Awali kwasababu ya miundombinu mibovu walikuwa
wanafika wamama wajawazito lakini ilkuwa inabidi tuwafikishe hospitali ya
jirani,lakini sasa haya majengo yamesaidia mpaka tumeongeza huduma, baada ya
huduma kupanuka na majengo kuongezeka tumeona hata kilinki akina mama
wameongezeka wakati ninafika walikuwa wanafika 15 kwa mwezi lakini sahizi
tumefika karibia hamsini”alisema Dkt,Rebeca Mduma
Aidha amesema licha ya kufanikiwa kupata vifaa mbali
mbali vinavyokidhi mahitaji ya kituo pamoja na majengo mapya laikini bado
wanakabiliwa na changamoto ya wauguzi pamoja na umeme.
“Changamoto nyingi zimetatuliwa na serikali iliopo lakini bado wauguzi ni
wachache na uongozi wa wilaya uliongeza wahudumu baada ya sisi kuanza huduma
hizi nyingine lakini pia changamoto zingine kituo kimekuwa kikubwa lakini
kunachangamoto ya umeme ambao tumekuwa tukipata kwa mgao”aliongeza Dkt,Rebeca
Mduma
Merry Mapunda ni mwalimu mstaafu na Gervas Mwinuka
ni muuguzi mstaafu wanaoishi kijiji cha Itundu kata ya Mlangali.Wanasema kituo
cha afya Mlangali kimekuwa na maendeleo makubwa kwenye utoji wa huduma za afya.
“Tumepata wataalamu bora zaidi ambapo zamani
tulitegemea vituo vingine lakini laeo tunafanyiwa hapa hapa na toka lianze
zoezi hili hatujaskia mama aliyepasuliwa akafa”alisema Merry Mapunda
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi
mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani
ya Chama hicho amefika na kukagua utoaji wa huduma katika kituo hicho na
kuridhishwa na watumishi jinsi wanavofanya kazi huku akiahidi kutoa mchango
wake wa kitanda kimoja kwenye wodi la mama na mtoto huku akichukua changamoto
zingine na kuzifikisha katika mamlaka zingine.
“Tumeona huko ndani vifaa tiba vya kutosha lakini
watumishi wa kutosha,na watumishi wa hapa hawalalamikiwi na wananchi hiyo ni
miongoni mwa mikakati ya Magufuli aliyoisimamia kwa maana ya kuleta nidhamu
serikalini”alisema Ngole
Vile vile Ngole amefika na kukagua maendeleo ya
ujenzi wa barabara ya Njombe-Ludewa kipande cha Lusitu-Mawengi inayojengwa kwa
kiwango cha zege na kuridhishwa na kasi ya ujenzi.
0 Comments