NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imeagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi
wote waliopewa mashine za kukusanyia mapao (POS) ambao hadi hivi wadaiwa
mapato waliyokusanya kwa kutoyawasilisha Benki.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Katibu Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa
kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Urambo.
Alisema kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha 60 cha Sheria ya fedha za umma yam waka 2001.
Makungu
alisema dosari za aina hiyo ndio zimekuwa zikisababisha upotevu wa
fedha za umma na kuziagiza Halmashauri kuhakikisha zinasimamia kwa ajili
ya kuziondoa.
Aidha
Katibu Tawala huyo wa Mkoa amepiga marufuku kwa Wakurugenzi na Waweka
Hazina kuruhusu utaratibu wa Wakusanyaji mapato kuchukua asilimia
zao(commission) kutoka makusanyo ya fedha za mapato ya ndani kabla ya
kupelekwa Benki.
Alisema
vitendo hivyo vinasababisha matumizi ya pesa ‘mbichi’ na kupelekea
Halmashauri kupoteza mapato yake na kusababisha uzalishaji wa hoja za
kiukaguzi.
Katika
hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora ameziagiza
Menejimenti za Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha hazizalishi
madeni yanayotokana na stahili za watumishi wanahama na wale
wanaopandishwa madaraja.
Alisema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishaagiza hakuna mtumishi
atayehamishwa bila kulipwa stahili na kuongeza kuwa kwenda kinyume cha
hapo ni kutenda kosa.
Makungu
aliongeza kuwa kuchelewa kulipa stahiki za watumishi kunavunja morali
ya kufanyakazi jambo ambalo linaweza kusababisha mgawanyiko miongoni mwa
Watumishi.
Aidha
Katibu Tawala huyo aliagiza Halmashauri zote kuanza kuandaa stahiki za
posho za Madiwani ili Mabaraza yatakapovunja wasipate usumbufu wa
kufuatilia.
0 Comments