Wakati msimu wa uvunaji wa matunda ya Parachichi
Ukiwa umewadia mkoani Njombe, wakulima wanaojishughulisha na kilimo hicho wameiomba serikali kuwasaidia wataalam
watakaowapa elimu ya kuondokana na changamoto inayopelekea
matunda kushambuliwa na wadudu na hivyo kushindwa kukidhi hitaji la soko la Dunia.
Kwa siku zinahitajika tani mia moja za parachichi zitakazonunuliwa na mataifa ya
Ufaransa na Dubai kutoka mkoani Njombe Ambapo juhudi za wakulima wa zao la
Parachichi zinaelezwa zinakumbana na changamoto ya matunda yao kushambuliwa na
wadudu shambani.
Baadhi ya Wakulima wa Tunda hilo ni Pamoja na Elina
Msemwa huku Felis Mgaya ambayeni Katibu wa Kikundi cha Wakulima wa Parachichi wamesema
bado zao hilo linaendelea kukabiliwa na changamoto kutokana na sasa kuwa zao
kimbilio mkoani Njombe.
Katika kijiji cha Mlevela wilayani Wanging’ombe
mkoani Njombe kikundi cha wakulima wa Parachichi cha KIWAMU chenye jumla ya
wanachama 78 ambacho kilianzishwa mwaka 2008 wakiungana kuuza matunda ya
parachichi kwenye ushirika,baadhi ya wakulima Akiwemo Bityseba Chengoma na
Julius Msigwa wanasema kufanya kazi za kilimo kwa pamoja kumewasaidia
kukabiliana na changamoto ambazo ni ngumu kushughulikiwa na mtu mmoja mmoja.
Jitihada za kutafuta masoko kwenye mataifa
mbalimbali ulimwenguni zinaelezwa zimekuwa na manufaa baada ya Asasi ya NSHIDA
inayowaunganisha wakulima wa matunda ya Parachichi mkoani Njombe Chini ya Mkurugenzi Wake Frank Mgaya kusaidia
kutafuta masoko,kuwashawishi wanunuzi wa matunda na kutoa bei nzuri kwa
mkulima.
0 Comments