Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe, anayemalizia muda wake wa Ubunge kupitia CHADEMA, na kisha kuendelea na chama chake cha sasa cha CCM, amesema kuwa kukosekana kwa ajenda muhimu za kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa 2020 ndani ya chama hicho, ndiyo chanzo cha yeye kutimkia CCM.
"CHADEMA watafute ajenda kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ujao sasa hivi hawana ajenda ndiyo kitu ambacho hata mimi kiliniondoa huko kwasababu sijaona ajenda inayotufanya tuende kwa wananchi kuomba kura, sasa hivi wamesha-shift kwenye mambo mengine yote wamebaki kulalama tu ooh mwambe amerudi Bungeni" amesema Mwambe.
Hivi karibuni Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, alieleza kutoitambua barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ya kulieleza Bunge kuwa lisimtambue tena Cecil Mwambe, kwa kuwa alishajiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama, badala yake Spika Ndugai alimtaka Mbunge huyo kurejea Bungeni.
0 Comments