TANGAZA NASI

header ads

CHADEMA washangaa kuitwa kushiriki tathmini ya uchaguzi

 





Na Amiri Kilagalila,Njombe


Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimesema hakipo tayari kuruhusu baadhi ya viongozi wake kushiriki katika kikao cha tathmini ya uchaguzi inayoelezwa kuandaliwa na Tume ya uchaguzi mkoani humo.


Akizungumza na mtandao huu,mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe Bi,Rose Mayemba amesema wamepata taarifa makatibu wao wa majimbo na wilaya kupigiwa simu za kushiriki tathmini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 28,2020.


"Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu waliojitambulisha kwamba wao ni Tume  ya uchaguzi wanawapigia simu makatibu wetu wa majimbo na wilaya za kuwataka wafike kwenye vikao vya tathmini baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.Hii sio sahihi"Alisema Rose Mayemba


Aidha mwenyekiti alihoji


"kuwalazimisha viongozi wetu kushiriki vikao vyao kunaleta sintofahamu kubwa.Wanataka nini?hiyo tathmini wanafanya majibu yake wanayapeleka wapi? kwanini leo na si mara tu ulipomalizika uchaguzi?"Alihoni Rose Mayemba 


Hata hivyo amesema kutokana na chama chao kufanyiwa hujuma katika uchaguzi huo na kutokuwa wa huru na haki,wamekubaliana kutoshiriki katika tathmini hiyo.


"Tumekubaliana makatibu wetu wasishiriki vikao vya tathmini ya uchaguzi.Tume ifanye tathmini na mabalozi na wasimamizi wa uchaguzi walioshirikiana nao kuharibu uchaguzi"Rose Mayemba mwenyekiti wa Chadema Njombe


Post a Comment

0 Comments