TANGAZA NASI

header ads

Wananchi watakiwa kuepuka kutupa hovyo taka zilizotumika kujikinga na Corona



Na Jackline Kuwanda, DODOMA.
DODOMA 
Wakazi wa jiji la Dodoma wametakiwa kutunza  mazingira hususani  katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 na kuepuka  kutupa hovyo  vifaa  wanavyotumia kujikinga na maambukizi  mara baada ya kumaliza kuvitumia.

 Wito huo umetolewa na  mkuu wa idara ya mazingira na udhibiti wa taka ngumu jiji la Dodoma  Bw. Dicksoni Kimaro ambapo amesema  licha ya mwamko mkubwa wa wananchi kutumia vifaa hivyo katika  kujikinga lakini wanapaswa kufahamu kuwa endapo watamaliza kuvitumia na kuvitupa  hovyo basi  watasababisha uchafuzi wa mazingira na kuleta madhara kwa viumbe wengine.

Amesema kila Mwananchi katika  makazi au eneo la biashara anapaswa kuwa na chombo maalumu cha kuhifadhia vifaa hivyo mara baada ya  kuvitumia ili kuepuka  uchafuzi wa mazingira.

Aidha Bw. Kimaro ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote na kufuata masharti yote yanayotolewa na wataalamau wa afya ili kuendelea kujinga na maambukizi ya ugonjwa wa Homa ya mapafu unaonezwa na virusi vya Corona.

Kwa upande wao baadhi ya wanachi wameelezea ni kwa namna gani wanahifadhi vifaa wanavyotumia kujikinga  mara baada ya kumaliza kutumia ambapo wamesema bado elimu zaidi inahitajika  kwa jamii kuhusu namna bora ya kutumia vifaa hivyo ambapo wamesema bado watu wengi mkoani humo hawana uelewa.

Kumekuwepo na mwamko kwa wananchi katika kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya  ikiwemo kutumia vifaa vya kujikinga umekua  mkubwa huku wakitakiwa kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi kwa kufuata utaratibu pasipo kuchafua mazingira.

Post a Comment

0 Comments