Na
Clief Mlelwa,Makambako
Waumini
wa madhehebu mbalimbali mkoani Njombe wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa
na wataalam wa afya na serikali kwa ujumla katika kukabiliana na virusi vya Corona
badala ya kuamini maombi pekee.
Hayo
yamesemwa na mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania usharika wa Mji Mwema mjini Makambako LYOSI MWALYOSI wakati
akizungumza na Ice fm,ambapo amesema kuwa waumini wote wanatakiwa kuchukua
tahadhili dhidi ya ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo ya watalaam wa afya badala
ya kuamini suala la maombi pekee.
Mchungaji
LYOSI amesema kuwa waumini wanatakiwa kuelewa kuwa hata maandiko matakatifu
yamesisitiza watu kuwa na maarifa,hivyo wasipofanyia kazi maelekezo hayo
ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa mikono kila wakati kwa
maji tiririka na sabuni wataangamia.
Aidha
mchungaji huyo amewataka wananchi kuhakikisha wazee,watoto na wenye magonjwa
hususani kisukari na HIV wanawekewa mazingira rafiki ya kujikinga na ugonjwa
huo kwa kuwa kupitia wataalam wa afya wamethibitisha kuwa makundi hayo yapohatiani
kupata maambukizi hayo.
Kwa
upande wao waumini wa kanisa hilo wameonyeshwa kuridhishwa na utaratibu wa kuwa
na misa tatu badala ya mbili za awali na kueleza kuwa hali hiyo itapelekea
wajikinge na maambukizi ya virusi vya corona.
0 Comments