Wananchi mkoani Manyara wametakiwa
kuwa makini katika kuzivaa barakoa pamoja na unawaji wa mikono pia
kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya ili kukabiliana na
ugonjwa wa virus vya corona ambao ni janga la dunia.
Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi
wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt.Catherin Mangali, wakati
akipokea vifaa kinga kutoka kwa Mbunge wa viti Maalumu Mhe. Ether
Mahawe.
Akizungumza katika makabidhiano ya
vifaa hivyo Dkt. Catherin alisema, janga la corona siyo kwa madaktari
pekee bali ni janga la kila mmoja hivyo namkushukuru mbunge huyo kwa
msaada wa vifaa kinga ili kukabiliana na virus hivyo.
Kwa upande wake Mbunge wa viti
Maalumu Mkoa wa Manyara Mhe. Ester Mahawe kwakushirikiana na umoja wa
wanawake wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Babati mjini wameweza
kukabidhi vifaa kinga kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara ikiwa ni
pamoja na Mandoo 20 kwaajili ya kunawia, lita 50 ya sabuni pamoja na
barakoa pc 500 na kusema kuwa lengo la msaada huo ni kwaajili ya
wangojwa wa wanafika hospitalini hapo ili kujikinga virusi vya corona.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Babati mjini [UWT] Bi. Gaudina
Eddan Hauli amesema kwa wakati huu madactari na wauguzi wapo katika
hatari kubwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona kutokana na
mazingira ya kazi zao kwani hukutana na watu tofautofauti wakati wa
kutoa huduma kwa wangonjwa hivyo nakuiomba jamii kuendela kumomba mungu
ili maambukizi yasiendelee kutokea.
0 Comments