Taariifa ya KNVB imesema kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali kuzuia mikusanyiko mikubwa, imekuwa vigumu kuumaliza msimu huu wa kandanda. Imesema afya ya umma ni suala la kipaumbele.
Vinara Ajax, ambao wako juu ya AZ kwa tofauti ya mabao, watafuzu katika ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa mujibu wa KNVB lakini watasubiri uamuzi wa shirikisho la UEFA mnamo Mei 25.
Hakuna timu itakayoshuka daraja wala kupandishwa daraja, na msimu ujao utaanza na timu 18 zilizokuwa katika ligi kuu msimu huu.
Chanzo:Muungwana Blog
0 Comments