TANGAZA NASI

header ads

Kenya waongeza marufuku ya kutotembelea mji mkuu



Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya watu kusafiri na kuingia au kutoka katika mji wa Nairobi na miji mingine minne kwa muda wa siku 21.

Marufuku ya kutoka nje kwa taifa zima pia imeongezwa kwa siku 21.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza marufuku ya kuingia na kutoka katika kaunti za Nairobi, Kilifi, kwale Mombasa huku taifa hilo sasa likiwa na visa 343 na wagonjwa waliopona ni 98.


Kuendelea kuepuka kukaribiana na kuzingatia ushauri wa kukaa mita mbili kutoka kwa mtu mwingine

Wasiwaweke hatarini watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na wenye magonjwa ya kudumu
Amewataka mafundi wa nguo kutengeneza barakoa nyingi na akasema maafisa wa afya watawaelekeza namna zinavyotengenezwa.

Gari lolote la mizigo halitaruhusiwa kuwa na watu zaidi ya watatu na inapaswa kuwa na kibali cha maafisa

Wizara ya afya nchini humo ilitangaza wazi kuwa kwamba inatengeneza barakoa ambazo zitasambazwa kwa wananchi hivi karibuni.

Wizara ya afya imeeleza kuwa watu watakaokufa kutokana na virusi vya Corona watazikwa ndani ya saa 24 huku watu wa karibu wa familia wasiozidi 15 wakiruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayoandaliwa na Serikali.

Aidha, ndege kutoka nchi za kigeni zimeendelea kipigwa marufuku kuingia Kenya kwa siku 30 zaidi.

Hatahivyo, marufuku hii iliondolewa kwa ndege za kigeni zinazokuja kuhamisha raia wa nchi za nje waliokwama ingawa zinatakiwa kutoa taarifa kwa serikali angalau saa 72 kabla.

Ndege zingine ambazo hazitaathirika na marufuku hii ni zile za kubeba mizogo hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa serikali inaagiza vifaa vya wahudumu wa afya kutoka nje.

Na kutokana na ongezeko hilo, kuanzia Jumatatu, matatu au daladala pamoja na bodaboda ambazo zitakiuka sheria zilizowekwa zitapokonywa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kusambaza virusi kimaksudi.

Post a Comment

0 Comments