MSEMAJI wa klabu ya soka ya APR na mchambuzi nguli wa michezo
kutoka nchini Rwanda, Clever Kazungu, amesema kuwa ana uhakika kama hali ya
mambo itakuwa nzuri na Ligi Kuu Bara kurejea basi mshambuliaji wa Simba, Meddie
Kagere atafunga mabao 30 msimu huu.
Kazungu amesema kuwa haoni uwezekano wa Kagere kukosa mabao 11
katika mechi ambazo Simba imebaki nazo.Simba imesaliwa na mechi 10 ili
kukamilisha msimu ambapo itacheza jumla ya mechi 38 na Kagere kwa sasa amefunga
mabao 19.
“Sina shaka na uwezo wa Kagere katika suala la kuwatungua
makipa, ni mchezaji wa viwango vya juu katika eneo la ushambuliaji.
“Naamini kama hali ya mambo itakuwa nzuri na Ligi Kuu Bara
ikarejea basi Kagere atafunga mabao 30 msimu huu, sioni uwezekano wa kukosa
mabao 11 katika mechi ambazo klabu yake ya Simba imesaliwa nazo,” alisema
Kazungu.
Kagere ambaye msimu uliopita aliibuka kinara wa upachikaji mabao
baada ya kuweka kambani mabao 23, anakaribia kuivunja rekodi hiyo, mpaka sasa
msimu huu amefunga mabao 19.
Chanzo:Salehe jembe
0 Comments