Na
Jackline Kuwanda, DODOMA.
Katika
kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa
na virusi vya Corona (COVID-19) ,Wananchi katika wilaya ya Rombo mkoani
Kilamanjaro wameendelea kuelimishwa juu ya namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya
ugonjwa huo.
Akizungumza
mkoani hapo,Mbunge wa Rombo Joseph Selasin amesema kuwa anaishukuru serikali ya
wilaya ya Rombo pamoja na serikali ya mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanya kazi
kubwa ya kuelimisha wananchi hao namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Wakati
huo huo Mbunge huyo amesema watu wamelipokea suala hilo kwa kuendelea kujikinga
na kufuata maelekezo yote ambayo yemetolewa na wizara ya afya.
Amesema
wananchi wake wako tayari kupokea ushauri wa serikali na wataalamu katika
kutekeleza hilo, kwani hiyo itasaidia kuondosha maambukizi ya ugonjwa huo.
Akizungumzia
hali ya utalii katika jimbo hilo,amesema sekta hiyo haijapata msukumo wa
kutosha.
0 Comments