DODOMA.
TUME ya taifa ya sayansi na teknolojia nchini,COSTECH imetoa
zaidi ya shilingi milioni 600 kwa kituo cha utafiti wa mifugo Mpwapwa
jijini Dodoma ili kufanya maboresho ya miundombinu kuongeza ufanisi katika
utendaji wao wa kazi utakaochangia wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa
unaoendana na soko Duniani.
Hayo yamesemwa na Dkt Eliakunda
Kimbi ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa mifugo, Mpwapwa jijini
Dodoma , wakati wa ziara iliyofanywa na tume ya taifa ya sayansi na
teknolojia (COSTECH) kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa miradi
inayosimamiwa na tume hiyo akieleza kuwa miongoni mwa majukumu yao ni pamoja na
upandikizaji wa viini tete vya ngo’mbe.
Dkt. Kimbi ameishukuru COSTECH kwa
kuishika mkono sekta ya mifugo akisema kwamba baadhi ya watu hushindwa kujikita
katika ufugaji kutokana na shughuli hiyo kuonekana kufanywa na makabila
fulani mtazamo ambao husababisha kuipa kisogo fursa ya ufugaji ambao
ukisimamiwa vyema ni wazi utachagiza sana maendeleo ya mfugaji na kuongeza pato
la taifa.
Pia amewataka wafugaji kuwa
wabunifu katika shughuli zao hatua itakayochangia uzalishaji wa mifugo
wenye tija kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu na kuongeza thamani ya mifugo
hiyo itakayokuza soko la mifugo kimataifa.
Dkt. Kimbi amesema zipo changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya ufugaji ikiwemo gharama za ufarishaji
wa viini hivyo kutoka afrika kusini na wakati mwingine huaribika,
mabadiliko ya tabia nchi, upungufu wa malisho ambazo mara nyingi
husababisha migororo ya wakulima na wafugaji huku akiwasihi wafugaji na
wanaotarajia kufuga kufuatilia kanuni za ufugaji kwa mujibu wa sheria ili kuwa
na ufugaji salama.
Akizungumzia shughuli za kituo hicho
mtafiti na msimamizi wa mradi Kabuni Thomas kabuni amebainisha kuwa kituo
hicho ni kati ya vituo saba vya taasisi ya utafiti wa mifugo nchini akiongeza
kuwa lengo la kuanzishwa kwa mradi ni kuboresha uzalishaji wa viini tete
vya ngo’mbe kuondokana na ufugaji uliozoeleka na kuhamia kwenye
uzalishaji wa kisasa wa upandikizaji wa mbegu unaoendana na teknolojia ya sasa.
0 Comments