TANGAZA NASI

header ads

Uongozi wa hospitali ya rufaa Dodoma wakanusha taarifa za kukosa barakoa




DODOMA 

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma imekanusha taarifa zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuhusu ukosefu wa barakoa za kutosha kwa watumishi wa hospitali hiyo .

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Ernest Ibenzi amesema kuwa taarifa iliyokuwa inasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na watumishi wa hospitali hiyo kukosa barako sio  za kweli.

Aidha, Dkt Ibenzi amesema kuwa katika hospitali hiyo wamekuwa wakigawa kila asubuhi barakoa za kutosha kwa watumishi wote. 

Wakati huo huo amesema katika kipindi hiki ambapo kuna ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19)  katika hospitali hiyo ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo  wamepunguza idadi ya ndugu ambao wanakwenda kuwatembelea wagonjwa hospitalini hapo.

Hatahivyo, Dkt Ibenzi ameendelea kusema kuwa katika ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma vifaa vyote vya kujikinga na virusi vya Corona  vipo na watumishi wote wanapata.


Post a Comment

0 Comments