Walimu wanaofundisha katika shule mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita, wamelazimika kukimbia makazi yao kwenye maeneo ya shule kutokana na kuchapwa mijeredi na wakati mwingine kujikuta wakiwa wamelazwa nje.
Hoja hiyo imeibuka katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita, ambapo Diwani wa Kata ya Kanyara, Mapande Enock amesema kuwa walimu wanapitia shida hiyo kutokana na imani za kishirikina.
Diwani huyo akaenda mbali zaidi akitaka nyumba hizo zijengwe uraiani na si kwenye maeneo ya shule ambayo anaona ni hatarishi kwa maisha ya walimu, kwani shule nyingi zipo mbali na makazi ya watu.
Modest Alpolnary ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, akakiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo akishauri jamii kuacha tabia ya kuwapiga na kuwalaza nje walimu kwani inaathiri mkakati wa Serikali wa kuhakikisha walimu wanaishi katika mazingira mazuri.
CHANZO:Muungwana blog
0 Comments