Na Gabriel Kilamlya,Njombe
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imewaonya wanasiasa
walioanza kujitokeza kwa wananchi kugawa zawadi kabla ya muda wa uchaguzi na
kutangaza kuto kusita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Akizungumza
na vyombo vya habari kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Domina Mukama wakati
akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha miezi mitatu ya
januari hadi machi amesema kuwa tayari kuna baadhi ya wanasiasa wameanza
kujitokeza kuwahonga wananchi kinyume cha sheria.
“Mwaka
huu ni mwaka wa uchaguzi,nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba
kuwachagua madiwani,Wabunge na Rais kwa mujibu wa katiba ya Nchi.Taasisi
imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaokiuka
sheria,kanunina taratibu za uchaguzi ambao wameanza kufanya kampeni za
kuwashawishi wananchi kabla ya muda unaotolewa kwa mujibu wa sheria”alisea
Mukama
Baadhi
ya wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa mkoani Njombe akiwemo Edwin Mwanzinga
na Alatanga Nyagawa wanakiri kuwa rushwa ina madhara makubwa katika chaguzi
mbalimbali lakini wametaka takukuru iangazie macho yao katika vyama vyote vya
siasa badala ya kujikita na vyama vichache ili hali uchaguzi unahusisha vyama
vyote.
“Sisi
kwenye chama chetu cha mapinduzi unapotaka kutoa msaada hutakiwi kutoa kwa
kificho,unatakiwa uwasilishe kwenye ofisi za chama upate utaratibu ukienda
tofauti na hapo inatafsirika ni rushwa vinginevyo usigombee”amesema Mwanzinga
“Kweny
chaguzi zipo dalili za rushwa ni vyema vyombo vya kiserikali katika kipindi
hiki vikafanya kazi kikamilifu kwenye vyama vyote”alisema Alatanga
Erasto
Ngole ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe na Rose Mayemba ni mwenyekiti wa CHADEMA
mkoa ambao nao wamewaonya wanachama wao wenye nia ya kugombea kwa kuanza
kukiuka kanuni kabla ya mchakato kutangazwa.
Mwezi
Oktoba mwaka huu Tanzania inatarajia kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu
utakaowahusisha madiwani,wabunge na rais hatua ambayo imetajwa kugubikwa na
vitendo vya rushwa katika kipindi kama hiki.
0 Comments