Na Masanja Mabula ,Pemba
JUMLA ya watu 79
waliokuwa wamewekwa karantini kwenye kambi ya Chasasa wilaya ya Wete
wameruhusiwa kutoka na kutakiwa kuwa mabalozi katika sehemu wanazoishi
kwa kuhakikisha wanaeneza elimu ya kujikinga na virusi vya Corona.
Hata hivyo kutoka watu hao ikawa furs kwa wengine 93 kuingia ndani ya kambi baada ya kuwasili wakitoa nje ya Kisiwa.
Mkuu wa wiaya ya Wete Keptein Khatib Khamis Mwadini aliwataka kuendelea kufuata masharti ya wataalamu wa afya.
Alisema elimu
waliyoipata wakati wakiwa karantini wakaitumie kwa ajili ya kujikinga
wao pamoja na jamaa zao juu ya virusi vya Corona.
“Leo mnatoka nawaomba sana mkawe walimu kwa jamii inayowazunguka lengo ni kuikinga na maambukizi ya virusi vya Corona”alisema.
Katibu Tawala
Wilaya ndogo Kojani Makame Khamis Makame aliwataka kuhakikisha
wanajiepusha na mikusanyiko ya watu hususani maswala ya kucheza mipira.
“Hapa tunazungumza
na kila mmoja anapiga makofi, lakini najua mkifika kwenu hasa wanaoishi
kisiwa cha Kojani utasikia jioni wako mazoezini jambo ambalo
halitakiwi”alisema.
Naye Afisa Afya
Wilaya ya wete Mwarabu Ali Nuhu akizungumza na wananchi hao alisema ni
vyema kila mmoja akahakikisha anafuata maelekezo yanyotolewa na
serikali.
“Hili janga lipo
na linaendelea kuitsa dunia , hivyo tunaaswa kuacha mazaha kwa
kuhakikisha wanaitumia vyema elimu waliyoipata wakati wakiwa ndani ya
kambi”alisisitiza.
Baadhi ya wananchi
wakizungumza baada ya kutoka karantini walisema kitendo cha wao kuwekwa
karantini kumewawezesha kupata taaluma na kuahidi kuifikisha kwa
wengine.
“Mwanzo nilipaniki
kuletwa hapa, kumba baada ya muda nilibaini kwamba kuna faida nyingi
ikiwemo pamoja na kuchunguzwa afya yangu”alisema Fatma Adam Othman wa
Kiuyu Kigongoni.
Hata hivyo watu
sita ambao waliingia Pemba wakitoka Kenya na Msumbiji wataendelea
kusalia karantini wakisubiri tamko la serikali.
0 Comments